Sanaa za Afrika ni shirika linalojitegemea ambalo lengo lake kuu ni kuhamasisha sanaa kama njia muhimu ya kuanzisha biashara ya nyumbani unao uwezo wa kuajira na kutengeneza mali. Soko za sanaa za kiafrika husaidia kuboresha uzoefu wa bidhaa za kiufundi kwa kuzifanya ziwe muhimu katika sekta rasmi ambayo ina uwezo mkubwa wa kuifanya nchi ipate fedha za kigeni zinazohitajika sana, na pia kusaidia kuboresha jamii na uchumi wa mafundi maskini na wale wa ngazi ya chini. Sanaa ya kiafrika ni shughuli inayo tambua umuhimu wa kuunganisha rasilimali za kiafrika na utamaduni wake ili kusaidia katika juhudi za kuimarisha msingi wa elimu, hivi kusababisha kutakikana kwa mazingira yanayo tunufaisha kwa njia mbalimbali.Sanaa ya kiafrika huonyesha mambo mbalimbali ya Sanaa ya Kenya inayo simamia utamaduni na maisha ya kila siku ya wakenya na waafrika kwa jumla. Utamaduni na Sanaa ni njia ya kipekee na huwakilishwa kwa desturi na mila, pamoja na watu wake. Utamaduni hutupa sisi wakenya mila ambazo tunafaa kuzitii kwa njia ya kujiwakilisha na kujielewa kwa uzoefu na kwa ujumla wa fikira zetu. Hii basi huwapa wakenya njia ya kujitofautisha kutokana na watu kutoka nchi zingine.Maonyesho ya ufundi na Sanaa ya afrika yanayo fanyika kila mwaka hujumuisha mafundi stadi wa Sanaa kutoka pande zote humu nchini. Onyesho hili huleta pamoja bidhaa tofauti kama vyombo vya kisanii vilivyo undwa kutokana na mbao, mavazi ya kiafrika, glasi, vifaa vya ngozi na mapambo ya nyumba. Vyote hivi huwa maonyeshoni yakiuzwa na hapa pia ndipo mahali ambapo unaweza kununua vyombo vya Sanaa ambavyo havipatikani kwa urahisi. Kenya pia hujulikana kwa ujuzi wake katika utengenezaji wa vikapu, mikeka, utamaduni na vifaa vinginevyo. Kwa haya, ufundi na Sanaa wa Kenya una soko linalo wavutia watali wa kutoka ngambo na pia wale wa kutoka humu nchini. |
Comments
Hide