Dialogue

Vocabulary (Review)

Learn New Words FAST with this Lesson’s Vocab Review List

Get this lesson’s key vocab, their translations and pronunciations. Sign up for your Free Lifetime Account Now and get 7 Days of Premium Access including this feature.

Or sign up using Facebook
Already a Member?

Lesson Notes

Unlock In-Depth Explanations & Exclusive Takeaways with Printable Lesson Notes

Unlock Lesson Notes and Transcripts for every single lesson. Sign Up for a Free Lifetime Account and Get 7 Days of Premium Access.

Or sign up using Facebook
Already a Member?

Lesson Transcript

Mji wa Eldoret
Mji wa Eldoret wa Kenya ni muhimu sana kama kituo cha serikali wa Mkoa wa Bonde la Ufa. Upo kusini pa milima Cherangani katika maeneo ya mwinuko zaidi ya futi 7000 juu ya usawa wa bahari. Hivi sasa, ni mji unaoendelea kwa kiwango cha kasi nchini Kenya. Pia ni nambari tano kwa ukubwa kwa miji yote Kenya.Eldoret inajulikana kwa mambo mengi ikiwa pamoja na soko lake maarufu na pia kiwanda chake maarufu cha kutengeneza jibini. Chuo kikuu cha Moi, cha kufunza na hospitali la rejeo zote zipo katika mji huu. Chuo cha Eldoret Polytechnic pia kiko huko. Aidha, viwanda vina jukumu kubwa kwa uchumi wa mji huo. Kuna idadi ya viwanda pia kama ushonaji wa nguo, kiwanda cha mahindi na ngano. Viwanda hivi vinavyotambuliwa kitaifa ziliazishwa na baadhi ya familia kongwe za Kihindi katika kanda hii.Mji huu mdogo pia huwa ni eneo la mafunzo wa wanariadha ikiwamo wanariadha wa Kenya wakiosifika. Ushindi wa mbio wa dunia kwa wanariadha wa sehemu hii umechangia pakubwa kwa uchumi wa mji huu. Sababu ambayo huifanya eneo hili kuwa pahali bora kwa mafunzo ya wanariadha ni kimo kirefu kutoka baharini. Ni vigumu zaidi kukimbia mbio ndefu katika eneo ya kimo kirefu kwa sababu ni vigumu kupumua. Jambo hili hufanya kukimbia katika miinuko ya chini kuonekana rahisi. Mji huu pia ni mahali pakuu pa Mafunzo ya Miinuko ya juu ya usawa wa bahari ya Shirikisho la Kimataifa la Riadha. Wanariadha wa Kenya na wa kimataifa huja Eldoret kwa mafunzo.

Comments

Hide