Dialogue

Vocabulary (Review)

Learn New Words FAST with this Lesson’s Vocab Review List

Get this lesson’s key vocab, their translations and pronunciations. Sign up for your Free Lifetime Account Now and get 7 Days of Premium Access including this feature.

Or sign up using Facebook
Already a Member?

Lesson Notes

Unlock In-Depth Explanations & Exclusive Takeaways with Printable Lesson Notes

Unlock Lesson Notes and Transcripts for every single lesson. Sign Up for a Free Lifetime Account and Get 7 Days of Premium Access.

Or sign up using Facebook
Already a Member?

Lesson Transcript

Mji wa Karatina
Karatina ni mji wa kisasa. Historia ya mji huu inaanza kama kituo cha masomo ya shule za upili zilizoanzishwa na wamishonari wa makanisa mbali mbali. Kama inavyojulikana, Mkoa wa Kati ulikuwa chemichemi ya masomo rasmi ya kwanza kufanywa nchini Kenya. Haijulikani hasa kwa nini wamishonari hawa walichagua eneo moja kufanya azma yao. Kati ya tarafa sita zilizomo kata ya Nyeri, Karatina ilikuwa na jumla ya mashule ishirini ikilinganishwa na mashule mawili katika tarafa jirani ya Othaya mnamo mwaka wa 1910. Yamkini, machifu wa eneo hilo hawakulieza masomo sana na hivyo basi waliungana na wazungu kujenga mashule ya watoto wao. Wakati haya yakifanyika, sekta zingine zinazoenda sambamba na masomo ziliaza kukita mizizi karatina. Punde si punde, kijiji kikageuka kuwa mji wenye biashara kabambe.Mji huu kwa sasa umekuwa kielekezo kwa miji mingine nchini kwa sifa zake za usafi wa mazingira na mipangilio mufti wa majengo yake. Kulingana na kumbukumbu za serikali, mji huu una uwezo wa kupitisha maono ya millennia tukifika mwaka wa 2030. Juzi meya wa Karatina, Bwana John Kamau, alitabiri kuwa mji huo una uwezo wa kuzalisha ushuru takriban million kumi kila wiki. Jambo la kutia moyo ni kuwa mji huu unajivunia kuwa na soko kubwa zaidi katika bara la Afrika. Soko lenyewe limejengwa kutumia usanifu wa kisasa an hivyo basi kuonekana ikiwa safi zaidi. Nafaka na mboga za kila huletwa kila uchao na wakulima wa eneo hilo na kusafirishwa hadi Nairobi. Mboga na matunda kutoka sehemu hii huuzwa Amerika, Ulaya na nchi za Mashariki ya kati.Kwa bahati mbaya, sehemu hii ina shida ya usalama. Kundi haramu liitwalo Mungiki huwanyanyasa wakazi wa eneo hii kila mara. Jitihada za serikali kukumbana na kundi hili zimeambulia patupu lakini huenda siku moja wakawezwa na mkono mrefu wa sheria.

Comments

Hide