Dialogue

Vocabulary (Review)

Learn New Words FAST with this Lesson’s Vocab Review List

Get this lesson’s key vocab, their translations and pronunciations. Sign up for your Free Lifetime Account Now and get 7 Days of Premium Access including this feature.

Or sign up using Facebook
Already a Member?

Lesson Notes

Unlock In-Depth Explanations & Exclusive Takeaways with Printable Lesson Notes

Unlock Lesson Notes and Transcripts for every single lesson. Sign Up for a Free Lifetime Account and Get 7 Days of Premium Access.

Or sign up using Facebook
Already a Member?

Lesson Transcript

Mji wa Kisii
Kusini mashariki mwa Kenya kama unaelekea Kisumu utapitia vitongoji vingi kabla ya kuwasili mji wa Kisii. Jina la mji huu lilibuniwa kutoka kwa kabila la Wakisii ambao humiliki asilimia kubwa mwa mji huo. Utaweza kuona nyanda zilizokuzwa kila aina ya nafaka na migomba . Kulingana na sensa ya 2009, mji huu ulikuwa na wakazi wasiopungua elfu tisini. Kwa miaka michache iliyopita mji huu umekua kwa kiwango kikubwa. Inaaminika kuwa mji huu ndio unaokua na kiwango cha juu zaidi nchini ukifuatwa na mji wa Thika. Wakati wa ukoloni, mji huu ulitumika kukuza majani chai na pareto ingawa umebadilika na kuingilia ukuzaji wa vyakula vya aina mingi. Mandizi ya eneo hilo yamesifika Afrika mashariki na eneo lililoizingira.Mbali na hayo, mji huu hutumika kama kituo cha masomo. Vyuo vikuu vimefungua matawi yao ili kunufaisha jamii ya Wakisii. Kwa maoni yangu, watu wa jamii ya Wakisii wameendelea kimaisha ingawa nawalaumu kwa kushikilia mila na desturi ambazo zimepitwa na wakati. Ni jambo ambalo hunihuzunisha kuona wasichana wa umri mdogo wakikeketwa kwa kisingizio cha kuhifadhi mila na desturi zao. Serikali ya Kenya imejaribu iwezavyo kukomesha tabia hii ya jadi kama njia moja ya kupunguza adhari za ukeketaji lakini tendo hili lingali linaendelea.Mji wa Kisii vile vile umeonekana kulemewa na masomo ya msingi kilingana na matokeo ya hivi majuzi ya mtihani wa darasa la nane. Kati ya shule za msingi zilizoshikilia nafasi mia moja za mwisho, Kisii ilikuwa na shule kumi na tano. Uchunguzi uliofanywa na shirika moja lisilo la kiserikali uligundua kuwa watoto wengi hutumika na wazazi wao kufanya kazi za nyumbani badala ya kuwa shuleni. Waziri wa elimu alitoa agizo la kukamatwa kwa mzazi yeyote atakayepatwa akifanya kitendo kama hicho. Ni lazima wazazi wa eneo waelewe kuwa masomo ya msingi ni ya lazima kama ilivyoelezwa katika katiba ya Kenya.

Comments

Hide