Dialogue

Vocabulary (Review)

Learn New Words FAST with this Lesson’s Vocab Review List

Get this lesson’s key vocab, their translations and pronunciations. Sign up for your Free Lifetime Account Now and get 7 Days of Premium Access including this feature.

Or sign up using Facebook
Already a Member?

Lesson Notes

Unlock In-Depth Explanations & Exclusive Takeaways with Printable Lesson Notes

Unlock Lesson Notes and Transcripts for every single lesson. Sign Up for a Free Lifetime Account and Get 7 Days of Premium Access.

Or sign up using Facebook
Already a Member?

Lesson Transcript

Mji wa Lamu
Lamu ni mji wa kale ambao unaweza linganishwa na miji mingine ya enzi hiyo kama vile Unguja. Mji huu umo Kaskazini mashariki mwa mji wa Mombasa na hukisiwa kuwa mojawapo wa miji ya kwanza ambayo Waswahili waliwahi kujenga. Kisiwa cha Lamu hivi maajuzi kimekuwa kwenye magazeti baada ya serikali ya Kenya na ile ya Uchina kuweka mkataba wa kujenga bandari itakayotumika na nchi jirani za Ethiopia na Sudan. Dhoruba kali ya mawimbi huipiga mji huu mara kwa mara. Pwani ya Lamu ni mojawapo ya vivutio muhimu nchini Kenya. Kinachowashangaza watalii wengi ni kihafidhina cha watu wa Lamu. Kwa karne zilizopita, wakaazi wa Lamu wamehifadhi mila na desturi zao hivi kwamba mji wenyewe umeonekana kupitwa na wakati. Kihistoria, punda wamekuwa ndio vyombo vya usafiri mjini huo. Cha kushangaza ni kuwa wakati miji mingine nchini inajivunia kukuwa na njia za kisasa za usafiri, punda wangali ndio tegemeo kuu ya usafiri wa binadamu na mizigo mjini Lamu. Kisa na maana? Mji wenyewe ulijengwa bila kuzingatia njia zozote za uhandisi wa mitaa. Kisiwa chenyewe kimezingirwa na nyumba kuu kuu ambazo zimepitwa na wakati. Ijapokuwa zingine kama vile nguzo zilizowekwa na Mreno Vasco Dagama ambazo huwa vivutio za watalii, mingi ya nyumba za Lamu zinahitaji ukarabati au kubomolewa.Ilikuwa jambo la kutatanisha wakati vugu vugu la vikundi vinavyodai kuwa Pwani si Kenya kufikiria kuwa watu wa Lamu wana uwezo wa kujistahimili kimaisha bila kushirikiana na kata za bara. Ukweli ni kuwa mji wa Lamu unategemea utalii peke yake ambao wakati mwingine huzorota na kupelekea uchumi kuenda chini. Kwa hivyo, mji wa Lamu unahitaji kutafakari jinsi utakavyoshirikiana na maeneo mengine nchini ili kubadilisha sura yake ya kale na kuonekana kama mji maridadi wa Pwani. Wapwani ni watu wanaosifika kwa uzembe na huenda maendeleo ya kisiwa cha Lamu yakalegea kwa muda mrefu iwapo njia mwafaka hazitazingatiwa kubuni jinsi ya kuendelesha kisiwa hicho. Bandari mpya ina uwezo wa kubandilisha maisha ya wakazi wa Lamu ingawa sharti waelewe kazi zitakazochipuka kutokana na kukamilika kwa bandari hiyo zinahitaji utaalam na ujuzi wa hali ya juu.

Comments

Hide