Maneno mengi yamesemwa kuhusu Nyeri. Kinachokuja kwa mawazo ya watu wengi wanaposikia Nyeri hasa si mji wenyewe, ila historia ndefu ya mji huo. Kila mwaka, maskauti kutoka pembe zote za dunia hukusanyika mjini humu kumuenzi mwazilishi wa kikosi cha maskauti duniani, Bwana Baden Powell. Baada ya kupigana vita vya kwanza vya dunia, Bwana Powell aliamua kukita kambi katika mji wa Nyeri. Aliishi huko hadi kufa kwake na ulikuwa jambo la kustajabisha ilipojulikana aliomba kuzikwa katikati ya mji huo. Isitoshe, malkia wa sasa wa Uingereza Elizabeth aligundua kifo cha babake Mfalme George akiwa amepanga ndani ya hoteli moja iliyomo mbugani Aberdares. Kulingana na gazeti moja ya London "Aliingia kwa hii hoteli akiwa binti wa mfalme na kuondoka akiwa Malkia." Hayo ndiyo yaliyokuwa maneno aliyoyasema mwandishi wa gazeti ya Times pindi tu ndege aliyosafiria Malkia Elizabeth ilipotua Mjini London.Mbali na hayo, mji huu umefahamika nchini Kenya kama kitovu cha mashujaa waliopigania uhuru wa nchi ya Kenya. Generali Kimathi na naibu wake Generali Mathenge ni wazaliwa wa mji wa Nyeri. Wakati wakoloni walipotambua rutuba na hewa safi ya nyanda za Aberdares waliwasili na wajukuu wao na kuufumania mji wa Nyeri. Kenya kwa zaidi ya nusu karne ilitawaliwa na serikali ya Uingereza lakini wakazi wa Nyeri waliamua kupinzana na sheria za unyanyasanji. Mau Mau ilibuniwa kama jeshi la waasi ambalo lilipigania uhuru wa Kenya. Makao yake makuu, operasheni na mawasiliano yalikyuwa Nyeri. Kufuatia kuimbuka kwa vita za pili za dunia, ilikuwa bayana kuwa wazungu walikuwa wamekubali kuzipa nchi za Afrika uhuru.Kwa wakati mrefu, kahawa iliyokuzwa nchini Kenya imesifiwa kwa ubora wake. Jambo la kuridhisha ni kuwa theluthi moja ya kahawa hii yenye sifa tele imekuzwa viungani mwa mji wa Nyeri. Marehemu profesa Wangaari Maathaui alizaliwa mjini Nyeri, akasomea mumo humo na baadaye akaanza harakati za kukomesha uharibifu wa mazingira. Jambo hilo la busara lilipelekea kamati ya Nobel kumtambua na kumtunza mwanamke huyu jasiri kwa tunzo lenye dhamani zaidi duniani, tuzo la amani mnamo mwaka wa 2004. |
Comments
Hide