Dialogue

Vocabulary (Review)

Learn New Words FAST with this Lesson’s Vocab Review List

Get this lesson’s key vocab, their translations and pronunciations. Sign up for your Free Lifetime Account Now and get 7 Days of Premium Access including this feature.

Or sign up using Facebook
Already a Member?

Lesson Notes

Unlock In-Depth Explanations & Exclusive Takeaways with Printable Lesson Notes

Unlock Lesson Notes and Transcripts for every single lesson. Sign Up for a Free Lifetime Account and Get 7 Days of Premium Access.

Or sign up using Facebook
Already a Member?

Lesson Transcript

Bonde la ufa
Bonde la ufa ni miongoni ya maajabu ya dunia. limetanda kutoka Mashariki ya Kati kupitia Afrika na kuteremka hadi nchini Msumbiji. Nchini Kenya, ufa huo unaweza tazamwa ukiwa Naivasha baada ya safari ya saa moja kwa gari kutoka Mji mkuu, Nairobi. Wanasayansi wananamini ufa huu ulitokana na kusuguana kati ya gandunia ya Uarabuni na ile ya Afrika. Msuguano huu ulipelekea gandunia la katikati kuzama na hivyo basi bonde la ufa kuumbwa. Baadaye, milipuko ya volkeno ilipelekea kuumbwa kwa milima kama Mlima Longonot. Vilindi vya Ziwa Tanganyika ndizo zenye kina zaidi duniani huku Ziwa Victoria likiwa ziwa la pili kwa ukubwa miongoni mwa maziwa yenye maji safi duniani. Maziwa haya mawili yamo katika bonde la ufa. Ziwa victoria ndilo chanzo cha mto Nile.Bonde la ufa lililo nchini Kenya lina chanzo chake Ziwa Turkana. Limegawanya nchi ya Kenya kwa urefu wake na kutengeneza baadhi ya maeneo ya kuvutia sana duniani. Ndani ya bonde la ufa kuna miinuko, majangwa, ardhi yenye rutuba na maziwa tele. Ziwa Turkana linaaminika kuwa makazi ya binadamu wa kale kulingana na wachimbaji visukuku. Mifuvu iliyochimbuliwa inakisiwa kuwa na miaka zaidi ya milioni mbili unusu.Kwa karne nyingi, bonde la ufa limetambulika kwa maeneo ya kuvutia mamilioni ya watalii wanaotembelea nchi ya Kenya. Baadhi ya mavutio haya ni aina mbalimbali za wanyamapori, volkeno zinazo uwezo wa kulipuka tena na zile zilizokamilisha milipuko yake, ndege wa aina mbalimbali na matenki ya maji moto ni kati ya maeneo mengi ya kutembelea. Kiuchumi, bonde hili ni kikapu cha nafaka za aina nyingi zinazokuzwa nchini Kenya. Asilimia sitini ya mahindi inayokuzwa nchini huvunwa kwenye sakafu ya bonde la ufa lenye rutuba. Matenki yenye maji moto huzalisha asilimia nane ya kawi nchini Kenya. Migodi ya madini kama vile chokaa na chuma huchibwa katika bonde la ufa. Ardhi yenye rutuba imewasaidia mamilioni ya watu wanaotegemea kilimo kijiendeleza kimaisha. Kenya inashikilia nafasi ya tano kati ya nchi zinazouza nje majani chai, nafasi ya kwanza kati ya nchi zinazokuza maua pamoja na nafasi ya kwanza duniani katika ukuzaji wa pareto. Zaidi ya asilimia themanini ya maua haya hukuzwa katika bonde la ufa huku asilimia arobaini ya majani chai inayouzwa nje mwa Kenya ikivunwa mumo humo.

Comments

Hide