Dialogue

Vocabulary (Review)

Learn New Words FAST with this Lesson’s Vocab Review List

Get this lesson’s key vocab, their translations and pronunciations. Sign up for your Free Lifetime Account Now and get 7 Days of Premium Access including this feature.

Or sign up using Facebook
Already a Member?

Lesson Notes

Unlock In-Depth Explanations & Exclusive Takeaways with Printable Lesson Notes

Unlock Lesson Notes and Transcripts for every single lesson. Sign Up for a Free Lifetime Account and Get 7 Days of Premium Access.

Or sign up using Facebook
Already a Member?

Lesson Transcript

Makumbusho Ya Reli Nchini Kenya
Makumbusho ya shirika la reli la Nairobi ni mojawapo ya maeneo ambayo ungependa kutembelea kila unapozuru Kenya. Makumbusho haya yako katika jengo la zamani linalopatikana katika barabara kuu ya Uhuru jijini Nairobi.Kuzuru Makumbusho haya ni kama kugeuza kurasa za kitabu cha historia cha zamani, utapata majibu ya maswali yote huhusu historia ya shirika la reli na jinsi limeendelea kukua . Kumbusho hili ambalo limetiliwa mkazo na watu wachache kuhifadhi rekodi za shirika la reli la Afrika Mashariki tangu lianze hadi kukamizika kwake.Maonyesho haya hujumuisha mabaki ya injini za mvuke, mifano ndogo ya treni na meli zilizotumika miaka ya tisini.Kuna picha zinazonyesha vile ujenzi wa reli uvyoendelea jinsi wengi wetu tulivyosoma katika historia.Makumbusho haya yana ramani zilizotumika katika enzi hizo,michoro ya zamani na pia magazeti. Michongo maridadi iliyotengenezwa nyakati hizo pia ni mojawapo ya hifadhi.Kando na kutoa historia ya reli,kabara hili yapata kujibu maswali yote kuhusu jiji la Nairobi, kuhusu ilivyoanza na jinsi ilivyoendelea kukua. Kama umekewa ukiponda jinsi jiji hili lilivyoanza,tembelea mkabara huu na utapewa maelezo yote. Nafasi ya kutembelea Makumbusho haya huwa wazi kwa watu wote na kiingilio ni kidogo zaidi ikilinganishwa na pesa zinazotozwa katika maeneo mengine yanayovutia watalii. Watu wazima wanapaswa walipe shilingi mia moja tu na watoto shillingi hamsini. Makumbusho haya hayatoi historia ya reli pekee mbali ya Kenya kama nchi kwa ujumla.

Comments

Hide