Dialogue

Vocabulary (Review)

Learn New Words FAST with this Lesson’s Vocab Review List

Get this lesson’s key vocab, their translations and pronunciations. Sign up for your Free Lifetime Account Now and get 7 Days of Premium Access including this feature.

Or sign up using Facebook
Already a Member?

Lesson Notes

Unlock In-Depth Explanations & Exclusive Takeaways with Printable Lesson Notes

Unlock Lesson Notes and Transcripts for every single lesson. Sign Up for a Free Lifetime Account and Get 7 Days of Premium Access.

Or sign up using Facebook
Already a Member?

Lesson Transcript

Ziwa Turkana
Kwa wale wanaotaka kupata uzoefu wa aina tofauti za mazingira, basi kwa hakika Ziwa Turkana ndipo pahali pa kuwa. Ziwa hili ni maabara bora kwa ajili ya utafiti wa jamii ya mimea na wanyama. Ni ziwa la uzuri wa aina yake, ambalo limezingirwa na milima ya volkano na inayoonekana kuwa na rangi ya zambarau kutokana na miale ya jua inayoiangazia kila wakati. Ziwa Turkana ambalo kitabo lilijulikana kama ziwa la Rudolf ni mojawapo ya maajabu ya asili ya ulimwengu ni ndilo ziwa kubwa zaidi linalopatikana jangwani katika dunia nzima. Ziwa Turkana limezungukwa na maji pembe tatu na unatumia mashua kuvuka ndio kufikia uvuo wake.Unatumia njia tofauti upande wa magharibi na upande wa mashariki kufikia ziwa hili kwa sababu pande hizi mbili zimegawanywa na bonde lenye umaarufu la suguta.ziwa hili huvutia wageni wengi sana kutoka duniani kote ingawaje liko katika mahali ambapo ni mbali sana kutoka mjini.Ziwa la Turkana lina hifadhi tatu za wanyama likiwemo mbuga la Sibiloi,hifadhi la kisiwa cha kusini na lile la kisiwa cha kati. Ziwa Turkana ni nyumbani kwa idadi kubwa zaidi duniani ya mamba wa aina ya nile, viboko, nyoka sumu na mamia ya ndege na samaki. Jamii zinazoishi karibu na ziwa Turkana hupata namna ya kuendeleza maisha kutoka kwa hili ziwa.Jamii hizi zina tamaduni za kuvutia mno na ambao huonyeshwa katika sherehe zinazofanyika kila mwaka.Sherehe hizi za kuvutia hujumuisha nyimbo za jadi na ngoma za kitamaduni kutoka jamii mbalimabali zinazoishi karibu na ziwa la Turkana.Hili ni jambo lingine ambalo huvutia watalii katika eneo hili kila mwaka. Pamoja na haya,ziwa hili pia lina mradi wa kuzalisha nguvu za umeme na inasemekana huwa inachangia takribani megawati mia tatu ya gridi za umeme unaotumika nchini.

Comments

Hide