Dialogue

Vocabulary (Review)

Learn New Words FAST with this Lesson’s Vocab Review List

Get this lesson’s key vocab, their translations and pronunciations. Sign up for your Free Lifetime Account Now and get 7 Days of Premium Access including this feature.

Or sign up using Facebook
Already a Member?

Lesson Notes

Unlock In-Depth Explanations & Exclusive Takeaways with Printable Lesson Notes

Unlock Lesson Notes and Transcripts for every single lesson. Sign Up for a Free Lifetime Account and Get 7 Days of Premium Access.

Or sign up using Facebook
Already a Member?

Lesson Transcript

Ngome la Yesu
Ngome la yesu hupatikana katika kisiwa cha Mombasa katika jimbo la pwani, Kenya. Lilijengwa na Ureno katika mwaka wa 1593. Ngome hili lilijengwa kwa madhumuni ya usalama wa maisha ya wareno nchini Kenya. Leo, ngome hili hutumika kama jumba la makumbusho. Umbo la ngome hili huiga mfano wa mtu, likitazamwa kutoka hewani, na lilipewa jina la Yesu. Umbo hili huonekana kama mtu aliyelala kwa mgongo, huku kichwa kikielekea baharini. Waarabu walilishambulia ngome hili kuanzia mwaka wa 1696 hadi 1698. Baadaye Waingereza walilibadilisha na kulifanya gereza, kuanzia 1895 hadi 1958, ambapo walilifanya jumba la kihistoria. Katika mwaka wa 1958, lilibadilishwa na kufanywa Hifadhi la Taifa. Maonyesho katika ngome hili huwa ni pamoja na matokeo ya utafiti kutoka Ngome lenyewe, Gede, Manda, Ungwana na maeneo mengineyo. Pia, Kuna vitu vingine vya maonyesho ambavyo vilichangwa na watu binafsi kama vile Bi JC White, Mheshimiwa CE Whitton na Bi WS Marchant. Ngome hili limeimarishwa vizuri ingawa limepitia hali mbaya ya hewa. Mnamo mwaka wa 2011, ngome hili lilitangazwa kama mahali pa urithi wa dunia na likatajwa kuwa miongoni mwa mifano bora zaidi ya uturumbishaji wa kijeshi wa Ureno wa karne ya 16. Leo, ngome hili huwavutia watalii wa ndani na nje. Pia hutumika kwa ajili ya mipango mbalimbali ya utafiti, maabara ya Uhifadhi, na Idara ya Elimu na Ofisi ya Hifadhi. Kuta zake huwa na urefu wa mita 18. Ureno walikuwa wamejenga kuta za urefu wa mita 15, lakini Waarabu waliongeza mita 3 walipolichukua.

Comments

Hide