Mbuga la wanyama la Hells Gate lipo kusini mwa Ziwa Naivasha na Kaskazini Magharibi mwa Nairobi nchini Kenya. Mbuga hili lilianzishwa mwaka wa 1984 na huwa na upana wa kilomita za mraba 68.25. Mbuga lilipewa jina lake katika mwaka wa 1883 na Fisher na Thompson, ambao walikuwa wasafiri. Mbuga hili lilipata jina hili baada ya maporomoko membamba katika mawe yaliyosimama ya kihistoria yaliyolisha binadamu katika Bonde la Ufa. Licha ya kuwa ndogo, mbuga hili ni maalumu kwa ajili ya aina yake mbalimbali ya wanyama pori na kwa ajili ya maeneo yake ya kuvutia. Pia huwa na volkano mbili ambazo ni; Olkaria na Hobleys. Kuna zaidi ya aina 103 za ndege katika mbuga hili. Nyani, fisi, paa Thompsoni, nyati wa Afrika na pundamilia pia hupatikana huko. Simba, chui, na duma pia wamekuwa wakionekana huko, ingawa kwa idadi ndogo. Hata hivyo, mbuga hili linajulikana kihistoria kama makao ya tai. Mbuga hili huwa na vituo msingi vitatu ikiwa ni pamoja na kituo cha Masaai cha utamaduni. Kituo hiki cha Masaai hutoa elimu kuhusu kabila la Kimasai, utamaduni na mila. Mbuga hili limo mita 1900 juu ya usawa wa bahari na lina hali ya hewa ya joto na kavu.Limo katika kaunti ya Nakuru. Umaarufu wa mbuga hili hutokana ukaribu wake na Nairobi na pia malipo ya kiingilio ni nafuu yakilinganishwa na malipo ya mbuga nyingine. Kutembea, kuendesha baiskeli, pikipiki na kambi hukubalishwa katika mbuga hili. Kambi hapa ni salama ingawa; hakuna uzio kati ya kambi na wanyama pori. Pia hakuna bunduki. Ni mojawapo ya mbuga mbili tu za taifa la Kenya ambapo haya huruhusiwa. |
Comments
Hide