Dialogue

Vocabulary (Review)

Learn New Words FAST with this Lesson’s Vocab Review List

Get this lesson’s key vocab, their translations and pronunciations. Sign up for your Free Lifetime Account Now and get 7 Days of Premium Access including this feature.

Or sign up using Facebook
Already a Member?

Lesson Notes

Unlock In-Depth Explanations & Exclusive Takeaways with Printable Lesson Notes

Unlock Lesson Notes and Transcripts for every single lesson. Sign Up for a Free Lifetime Account and Get 7 Days of Premium Access.

Or sign up using Facebook
Already a Member?

Lesson Transcript

Siku ya Jamuhuri.
Mnamo Disemba 12 1963, serikali ya Uingereza ilitangaza kuondoka kwake katika ardhi ya Kenya na hivyo basi Kenya ikawa nchi huru. Vita vilivyo sababisha umwagaji wa damu zikawa zimeisha na Wakenya wakaanza kutayarisha kujitawala. Hayati Jomo Kenyatta akachukua wadhifa wa kuwa Rais wa Jamuhuri ya nchi changa iliyozaliwa. Tangu, Wakenya wamekuwa wakisherehekea kuzaliwa kwa nchi yao kila mwaka. Katiba iliyopitishwa pia iliweka kipengele cha kuhifadhi desturi ya kuifanya siku hii iwe sikukuu. Maelfu ya Wakenya wanaoishi Nairobi hukusanyika katika uwanja wa Kimataifa wa Nyayo kuhudhuria sherehe hii ambayo huongozwa na Rais wa Jamuhuri. Sherehe hii hujaa na mbembwe na michezo. Paredi ya wanajeshi pia hufanya kuonyesha umashuhuri wa nchi kupitia mavazi ya wanajeshi, wanapolisi, huduma ya taifa ya vijana na wanaskauti. Sherehe hii pia husheherekewa katika wilaya zote nchini ambapo makamishna wa wilaya na wakazi wa wilaya husherekea katika wilaya zao. Masuala mbalimbali kuhusu mambo muhimu kama vile usalama wa ndani, kilimo na masomo hujadiliwa. Kilele cha maadhimisho haya huwa hotuba ya Rais kwa wananchi wa Kenya. Rais pia huwatuza watu mbalimbali kwa juhudi zao za kufanya nchi iwe pahali bora pa kuishi. Mashujaa wa Uhuru husifiwa kwa kujitolea kwao kwa uanzilishi wa utawala wa kibinafsi nchini. Baadhi ya waliopigania Uhuru hualikwa katika ikulu kwa chakula cha jioni pamoja na Rais.

Comments

Hide