Dialogue

Vocabulary (Review)

Learn New Words FAST with this Lesson’s Vocab Review List

Get this lesson’s key vocab, their translations and pronunciations. Sign up for your Free Lifetime Account Now and get 7 Days of Premium Access including this feature.

Or sign up using Facebook
Already a Member?

Lesson Notes

Unlock In-Depth Explanations & Exclusive Takeaways with Printable Lesson Notes

Unlock Lesson Notes and Transcripts for every single lesson. Sign Up for a Free Lifetime Account and Get 7 Days of Premium Access.

Or sign up using Facebook
Already a Member?

Lesson Transcript

Tamasha za muziki
Tamasha za muziki nchini Kenya ni miongoni ya matukio makubwa katika kalenda ya Kenya.Tamasha hizi zimekuwa zikifanyika kutoka jadi hata kabla ya Kenya kujinyakulia uhuru.Sherehe hizi huandaliwa na serikali ya Kenya kupitia Wizara ya Elimu. Wanafunzi kutoka mashule mbalimbali na makoleji hushindana katika aina mbalimbali ya miziki hasa miziki ya asili na ngoma kutoka jamii mbalimbali za Kenya. Hizi sherehe hutoa nafasi bora kwa wanaoshiriki na watazamaji kusherehekea utamaduni wao na pia kuduumisha. Kupitia maonyesho mbalimbali, hasa ngoma na michezo ya kuigiza, na pia mavazi yanayovaliwa, wakenya hupata taswira ya jinsi maisha yalivyokuwa karne kadhaa zilizopita. Lengo kuu ya tamasha hizi ni kukuza uchezaji wa ngoma, maigizo, muziki, sarakasi, na elimu kwa maendeleo ya kijamii na binafsi. Tamasha hizi pia huendeleza sanaa ya utamaduni na ubunifu kupitia taarifa ya utendaji, na burudani. Sherehe hizi huvutia maelfu ya washiriki kutoka shule na pia taasisi za elimu ya juu. Hizi sherehe hufanyika kila mwaka kutoka mwezi wa Mei hadi Agosti. Wanaoshiriki hushindana kutoka ngazi ya tarafa hadi ya kitaifa katika makundi mbalimbali ya mizik ikiwemo ya ‘jazz, miziki za kihindi na ya aina ya ‘rap’ . Tamasha za kitaifa hufanyika katika mwezi wa Agosti kila mwaka katika jumba la kimataifa la mikutano la Kenyatta na huchukua takribani juma nzima. Hapa wakenya hupata matubuizo kutoka kwa nyimbo na densi zilizoibuka bora zaidi. Miziki ya zilizopedwa hasa benga ambao ni maarufu zaidi huwafurahisha wengi katika tamasha hizi. Waliohudhuria hupata vijitabu kueleza maana ya maonyesho mbalimbali ambayo hufanyika katika lugha za kiasili. Hii ni njia nzuri ya kukuza umoja miongoni mwa makabila mbalimbali nchini Kenya. Washindi katika nyanja mbalimbali hutuzwa katika kilele cha tamasha hii.waliong’aa zaidi huandaliwa karamu na kumtubuiza rais katika ikulu ya kenya. Hili ndilo jambo ambalo kila mmoja anayeshiriki tamasha hizi hutazamia.

Comments

Hide