Dialogue

Vocabulary (Review)

Learn New Words FAST with this Lesson’s Vocab Review List

Get this lesson’s key vocab, their translations and pronunciations. Sign up for your Free Lifetime Account Now and get 7 Days of Premium Access including this feature.

Or sign up using Facebook
Already a Member?

Lesson Notes

Unlock In-Depth Explanations & Exclusive Takeaways with Printable Lesson Notes

Unlock Lesson Notes and Transcripts for every single lesson. Sign Up for a Free Lifetime Account and Get 7 Days of Premium Access.

Or sign up using Facebook
Already a Member?

Lesson Transcript

Mbio za Lewa marathon
Mbio za nyika ya Lewa imetambulika kama mojawapo ya mbio yenye ugumu zaidi humu duniani. Ni mashindano ya kila ambayo hufanyika katika mbuga la Lewa ambalo liko kilomita mia mbili thelathini na tatu kutoka Nairobi na liko futi elfu moja mia tano juu ya usawa wa ufuo wa bahari. Mbuga la Lewa liko maili mia moja kutoka kwa ikweta pahali ambapo joto huenda likazidi digrii thelathini na saba kwa mwaka mzima. Joto jingi na usawa wa ufuo wa bahari huwatisha hata wale walio na uzoefu wa mbio hizi za masafa marefu. Mashindano huhisaniwa na Safaricom wakishirikiana na shirika la wanyamapori la Lewa kwa ajili ya kukusanya pesa ili kunufaisha vitongoji vilivyo karibu na mbuga hili na pia kuhifadhi wanyama wa pori. Mbio za nyika za Lewa ni vya kipekee kwa vile vinatendeka ndani ya mbuga hili ambapo mna wanyama pori kama vile; ndovu, simba,nyati na kifaru. Humu hamna kuta za kuwatenganisha wanyama pori na wanariadha hawa, hili ni jambo ambalo laweza kuleta utata katika hadhi ya usalama. Hata hivyo, maafisa wa usalama wakiwa pamoja na wanashirika wa wanyama pori, walio na ujuzi wa kutumia silaha, huhakikisha usalama kwa wakimbiaji kwa kulinda njia zinazotumiwa na wanariadha hawa. Tukio hili la kukata na shoka limeendelea kuwapa motisha wakimbiaji wa mbio za nyika na pia mashabiki. Wakimbiaji wanaojimudu kwa njia tofauti hujitokeza duniani kote kuanzia wanaotaka kujiburudisha, mashabiki hadi mabingwa kama Paul Tergat wa Kenya aliye shikilia rekodi ya dunia. Safari yote hua ni mzunguko wa kilomita ishirini na moja kwa barabara ya vumbi inayotumikiwa na magari ya kutalii katika mbuga hii. Mbio kamili ya nyika huwa ni mizunguko miwili na ule wa mzunguko mmoja ni nusu marathon. Mbio hizi huwa si za kulazimishwa. Kuna watu ambao wanaweza kukimbia mbio zote na wale wanaojimudu nusu marathon. Pia kuna mashabiki wanao washangilia wengine. Baada ya mashindano haya makubwa, maadhimisho ya kufuata mbio hufanyika ambapo wanariadha na mashabiki hujiandalia sherehe kwa mathumuni ya kujiburudisha.

Comments

Hide