Tamasha za usimulizi hadithi za kitaifa za Sagana ni za lazima kuhudhuria kwa wanaopenda hadithi na fasihi. Hizi sherehe huvutia washiriki kutoka India, Marekani, Ubelgiji, Uswizi, Uganda Tanzania yakiwemo mataifa mengine. Pia huleta pamoja wasimulizi hadithi mashuhuri kutoka kote ulimwenguni wakiwemo Dianne Farlote kutoka Marekani, Jeeva Rughanath kutoka India na wasanii wenye vipaji kutoka Kenya. Burudani hii ambayo huchukua siku tatu ilifanyika kwa mara ya kwanza nchini kenya katika mwaka wa 2009 na hufanyika kila mwaka kati wa mwezi wa Juni na Julai katika jumba la ‘Alliance française’ jijini Nairobi. Tamasha hizi huandaliwa na shirika la ‘zameleo culture and arts trust’ . Tamasha hizi hulenga kuendeleza utamaduni wa sanaa wa hadithi kupitia mawasiliano mbalimbali kwa kutumia maneno, muziki na ngoma. Hadithi ambazo hutolewa huwa na nia ya kuelimisha, kuweka maadili, kuhifadhi utamaduni na kuburudisha. Tamasha hizi zina burudani kwa watu wa umri wote, wazee kwa vijana na huguzia maswala mengi yanayowahusu. Watu kutoka kote duniani hukusanyika kuhadithia tamaduni zao mbalimbali. Kupitia mawasiliano mbalimbali, tunapata nafasi ya kushiriki katika utajiri wa sanaa za mila tofauti kwa mitindo ya kisanaa.Tamasha hizi pia huguzia maswala yanayosaidia watu kujielewa, jinsi ya kuyatunza mazingira, siasa za utawala na uhusiano katika jamii. Kuna pia mawasilisho mengine juu ya hadithi za kale za Ulaya na Afrika, hadithi kuhusu mapambano na ushindi na zile ambazo zinahusu maisha ya kila siku ya binadamu . Kando na usimulizi hadithi, tamasha hizi pia huhusisha mawasilisho mengine kama nyimbo na densi ili kuyafanya yawe ya kuvutia zaidi.Tamasha hizi hubeba mada fulani na ambayo huwa tofauti kila mwaka. |
Comments
Hide