Dialogue

Vocabulary (Review)

Learn New Words FAST with this Lesson’s Vocab Review List

Get this lesson’s key vocab, their translations and pronunciations. Sign up for your Free Lifetime Account Now and get 7 Days of Premium Access including this feature.

Or sign up using Facebook
Already a Member?

Lesson Notes

Unlock In-Depth Explanations & Exclusive Takeaways with Printable Lesson Notes

Unlock Lesson Notes and Transcripts for every single lesson. Sign Up for a Free Lifetime Account and Get 7 Days of Premium Access.

Or sign up using Facebook
Already a Member?

Lesson Transcript

Siku ya Madaraka
Kenya imejipa madaraka! Hicho kilikuwa kichwa cha habari katika gazeti la The Standard tarehe 12 Januari 1963. Mwaka mmoja baadaye Kenya ilipata uhuru wake. Babu yangu aliniambia, alikuwa akitembea siku moja jioni akitoka kwa shamba la mlowezi aliposikia habari hii njema kwa redio ya jamii. Katika siku hizo za kisiasa tele, watu walipaswa kutembea huku wamevaa kibandiko kilichokua na jina lake kwa shingo. Mmenyuko wa kwanza baada ya habari hiyo ilikuwa kutoa kibandiko hicho kilichojulikana kama ‘Kibandiko cha mbwa’ na kukitupa motoni lakini babu yangu alitafakari kwanza. Akajiuliza kama habari hiyo ni ya kweli? Saa moja baadaye, Sauti ya Kenya ilipeperusha hewani sauti iliyojulikana vizuri ya marehemu Jomo Kenyatta, Waziri Mkuu mpya wa Jamhuri ya Kenya. Waafrika wachache walikuwa wamelimika nyakati hizo. Chini ya asilimia tano ya wakenya wangeweza kutofautisha kati ya utawala wa kujitegemea na uhuru. Sherehe zikaanza mara moja hasa katika miji mikubwa. Shule zilipewa wiki moja ya likizo. Majadiliano katika barabara ya kujilimbikizia yalilenga suala moja: utawala binafsi. Maadhimisho zaidi yaliweza kupanuliwa kwa wiki zaidi. Wakenya waliingia mitaani kushangilia uhuru wao. Nyimbo zao zilikuwa za kuwasifu mashujaa wa vita. Waliwasihi mababu zao kubariki ardhi yao. Tangu wakati huo, siku hii imebakia siku muhimu kwenye kalenda ya Kenya na Afrika kwa ujumla. Wakenya husherehekea mtindo wa kipekee. Gazeti la serikali limeitaja sikuu hii kama likizo ya Taifa na marais wa mataifa jirani hufanya ziara kuheshima siku hii wakati wa kumbukumbu yake. Ni siku ya kutafakari tena wakati historia ya Kenya inaandikwa upya.

Comments

Hide