Dialogue - Swahili

Hide

Vocabulary (Review)

Hide
kuchukua to occupy
pango cave
uhuru independence
kilele climax, peak
Kundi la Mifugo herd
mashujaa wa uhuru freedom fighters

Lesson Notes

Hide

Cultural Insights

Did you Know?


 

There is a rich history associated with the Aberdares. It is said to be among the hide outs used by Mau Mau fighters in the struggle for independence. The famous freedom fighter Dedan Kimanthi used this forest as his post office and there is a giant tree where the freedom fighters would live messages for Kimanthi's attention in cases of emergency though it is hard to understand how the messages were left because the people then did not know how to read and write. There are also queen caves where the fighters used to preserve their meat. This is also a place where the kikuyus believed to be one of the habitats of Ngai (God).


 

Mlima wa aberdare una historia yenye utajiri mkubwa. Inasemekana ni kati ya maficho yaliyotumiwa na kundi la mau mau walipokuwa wakipigania uhuru wa taifa hili. Shujaa maarufu Dedan kimanthi alitumia msitu huu kama posta yake na inasemekena kulikuwa na mti mrefu ambapo mashujaa wengine walimuachia kimanthi ujumbe ingawaje ni vigumu kuelewa jinsi walivyo acha hizo jumbe maanake wengi wao hawakujua jinsi ya kusoma na kuandika. Kuna pia mapango ambayo yalitumika na mashujaa hawa kuhifadhia nyama walizotumia kama chakula. Msitu huu pia ni mojawapo ya maeneo ambayo kabila la wakikuyu waliamini ni makazi ya Ngai (Mungu)

 

Lesson Transcript

Hide
Mbuga La Wanyama La Aberdare.
Mlima wa aberdare uko katika nambari ya tatu kati ya milima ambayo ni mikubwa sana nchini kenya na unapatikana katika Kenya ya kati.Mlima huu una vilele viwili ambavyo urefu wake ni mita 4300 juu ya usawa wa bahari .Vilele hivi hufanya mabonde yenye umbo inayofanana na herufi “V” na kuna mito ambayo inapitia juu ya mabonde haya. Hii hufanya mlima huu uwe mahali bora kwa wapenzi wa mazingira. Kwenye eneo la juu ya mlima huu ni mbuga maarufu la Aberdare ambalo ni miongoni mwa maeneo makubwa ya kivutio cha utalii nchini. Hifadhi hii imechukua eneo kubwa ya mlima huu ikichukua takribani 767 mita kupiga mraba kati ya hekta 103,300 kwa ujumla. Makundi ya tembo na nyati ni miongoni mwa wanyama wengi ambao utapata katika harakati zao wakipita kwa kimya ndani ya msitu huu. Wanyama ambao hupatikana kwa urahisi katika mbuga hili ni pamoja na vifaru weusi, chui, nyani weusi na weupe, kima punju na tumbili wa aina ya ‘syke’. Upande wa juu wa msitu ni ukanda wa msitu wa mianzi ambao unakupa fursa ya kuona bongo, aina nadra ya swala anayeishi katika misitu ya mianzi. Msitu huu pia una zaidi ya aina mia mbili hamsini za ndege na utapata nafasi nzuri ya kuwatazama.Kuna makumpuni ya utalii ambayo yatakutembeza ndani ya mbuga hili kwa magari yao yakifahari ama pia unaweza zunguka kwa miguu. Kama mnazuru mbuga hili katika kikundi,mnaweza chukua nafasi hii kupiga kambi katika maeneo mazuri ya kambi na kukaa hapa kwa muda mtakaopendelea. Shughuli nyingine ambazo unaweza kushiriki ni pamoja na kukwea mlima au uvuvi katika mito inayopatikana katika eneo ya mlima huu. Mlima huu pia una vyumba kadhaa vya malazi ambamo wanaouzuru wanaweza pata mahali pazuri pa kupumzika.