Dialogue

Vocabulary (Review)

Learn New Words FAST with this Lesson’s Vocab Review List

Get this lesson’s key vocab, their translations and pronunciations. Sign up for your Free Lifetime Account Now and get 7 Days of Premium Access including this feature.

Or sign up using Facebook
Already a Member?

Lesson Notes

Unlock In-Depth Explanations & Exclusive Takeaways with Printable Lesson Notes

Unlock Lesson Notes and Transcripts for every single lesson. Sign Up for a Free Lifetime Account and Get 7 Days of Premium Access.

Or sign up using Facebook
Already a Member?

Lesson Transcript

MAISHA YANGU GEREZANI
Kitabu hiki kimeandikwa na John Kiriamiti aliyezaliwa tarehe 14 Februari mwaka wa 1950 Murang'a, nchi Kenya.
Alikamatwa na kupelekwa gerezani kwa miaka ishirini ambapo aliweza kuandika riwaya zake zinazo tambulika.
Riwaya hii inaanza na Jack Zollo anapowasili katika Mahakama ya sheria ya Nairobi ambapo alihukumiwa kifungu cha miaka ishirini gerezani na mijeledi arobaini na nne.
Jack anaudhika zaidi kwa muhula aliopewa huko jelani kiasi kuwa anazua vurugu nakuanza vita na askari wa jela na pia na wafungwa wenzake.
Anajifanya kana kwamba yeye ni mwenda wazimu ambapo analazwa katika taasisi ya akili kwa sababu ya ile hali yake ya wazimu na baadaye anatoroka kutoka kwa hospitali ya akili ya Mathare.
Hata hivyo, uhuru wake unadumu masaa kidogo tu ambapo anakamatwa tena na kurudishwa gerezani.
Jambo hili halimvunji moyo Jack Zollo ilhali anajitia moyo kuishi maisha magumu jelani anapokula kiazi kimoja kwa siku.
Jelani, Zollo anasimulia vituko vyake na vile mara kwa mara alivyokuwa kwenye vita na mawakala wa nchi na vile alivyoshinda jiji.
Ingawa mjini inambidi atoroke mara kwa mara maajenti wa sheria na wa amani ili aweze kuepuka kurushwa gerezani,
Zollo anaonekana mwenye kusherehekea maisha mazuri jelani na kuamua kuendelea kuishi pale gerezani licha ya ugumu.
Ana kuwa mashuhuri jelani kwa wafungwa wenzake na askari wa jela.
Kuongezea, anakuza ujasiri wake katika maishani yake ya jela.
Anatoka gerezani kama mtu aliyefanikiwa jelani na jijini huku akihusisha umaarufu wake kwa kuwa jambazi kabambe.
Jela linakuwa jiji kwa Zollo.
Kwake hakuna mpaka kati ya jela na jiji.

Comments

Hide