UVUKO WA DARAJA |
Mwangi Gicheru ni mwandishi wa kitabu hiki ambacho kina wahusika wa kuu watatu ambao ni; Karolina, Chuma na Kihuthu. |
Kihuthu ni babake Karolina. |
Chuma ni msimulizi na mfanyikazi wa familia ya Kihuthu. |
Kihuthu ni tajiri wa kupindukia. |
Karolina alianza mapenzi na Chuma, lakini jua kwamba wazazi wake hawangemruhusu aolewe na Chuma kwa ajili hali yake ya kijamii ilikuwa ya chini. |
Karolina alishika mimba ya Chuma, jambo lililowaaibisha familia yake. |
Chuma alijihurumia kwa ajili ya hali yake na wakati mwingine kujiona kama takataka ya kiwanda. |
Alidhani kwamba Mungu alimuumba baada ya chakula cha mchana kwa kutumia mabaki ya viumbe. |
Alidhani kwamba fedha ingeweza kumnunulia chochote. |
Alidhani kwamba babake Karolina hangekuwa na tatizo naye kama angelikuwa na fedha. |
Chuma alijuta kukutana na Kihuthu kwani aliona kama hili jambo lilimletea taabu. |
Hivyo basi akaanza kujihushisha na wizi ili kumfurahisha Karolina. |
Kwa bahati mbaya alipatika na akafungwa jela. |
Karolina alitorokea kijijini ambako maisha yalikuwa magumu. |
Baada ya kushikwa kwa Chuma, aliamua kurudi kwa familia yake. |
Jelani, Chuma alikutana na Kisinga ambaye alimwingiza katika ujangili baada ya muhula wao jelani. |
Chuma alienda Mombasa kumtafuta Karolina na kule kumwibia mtalii. |
Kisinga alikamatwa na kufungwa jela tena. |
Baadaye, Chuma alimpata Karolina ambaye alijaribu kumkimbia. |
Alianguka kwenye gazi, kitendo kilichofanya Chuma ashtakiwe kwa jaribio la wizi na uaji. |
Je, Chuma atafanikiwa kulivuka daraja la umaskini hadi utajiri? Mwangi Gicheru anaelezea maisha ya Chuma kwa kuchanganya upendo, furaha na utajiri. |
Comments
Hide