Wahu |
Wahu Kagwi ni mwimbaji Mkenya anayejulikana sana kwa jina Wahu. |
Sasa, yeye ndiye msanii bora wa kike katika burudani nchini. |
Ameoleka kwa mshindi wa tuzo katika uimbaji, Bwana Nameless. |
Pamoja wanabinti kwa jina Tumiso Nyakwea aliye na miaka karibu sita. |
Wahu alikuwa modeli na mhitimu wa hesabu katika chuo kikuu cha Nairobi. |
Alizaliwa mwaka wa 1980 na kuanza kazi ya mziki mnamo wa mwaka 2000. |
Nyimbo zake za kwanza ni zikiwemo Niangalie', 'esha' na ‘liar'. |
Hata hivyo, wimbo iliyofanya kuvuma zaidi ni ‘sitishiki' alitoa mwaka wa 2005. |
Wahu amepokea tuzo kadhaa baadhi yao ikiwemo msanii bora wa kike katika mashindano ya MTV Africa Music Awards mwaka wa 2008. |
Pia amesajiliwa kushiriki katika tamasha za MOBO na KORA mwakani 2008 . |
Alitunukiwa tuzo kama msanii bora wa kike katika tamasha la Pearl of Africa Music Award katika mwaka huo huo. |
Kando na kuimba, yeye pia ni mfanyabiashara. |
Juzi amefungua Saluni katika eneo la westlands Nairobi katika ghorofa ya chini la jumba la Krishna. |
Inasemekama kuwa yeye ndiye mwimbaji maarufu wa hivi juzi kufungua bishara ili kuongeza mapato yake. |
Maono yake alipokuwa akifungua saluni hii ni kuanzisha mahali ambapo urembo na nywele ya wanaume and wanawake wa Afrika utaeleweka na pia kutowa ushauri jinsi ya kulinda nywele na ngozi bila kujali rangi au mfumo. |
Wahu pia ni mratibu wa matukio katika Chuo Kikuu cha Nairobi katika kutano ya Metro, ambapo kazi yake ni kuandika na kutuma mapendekezo, kupanga matukio na mikutano ya watu. |
Yeye ni mpenzi wa maisha na urembo. |
Ameonekana katika majarida tafauti na watu kadhaa wamemtaja yeye na mumewe Nameless kama familia ya kwanza katika sekta ya muziki. |
Comments
Hide