Daddy Owen |
Daddy Owen ni mmojapo wa wasanii walionawiri sana katika uwanja wa muziki wa injili. |
Kwa sasa yeye ndiye mwanamuziki mbora katika uwanja huu. |
Jina lake rasmi ni Owen Mwatia lakini anajulikana kwa jina la usanii yani Daddy Owen. |
Baadhi ya watu pia humjua kama 'king of kapungala' huku wengine wakimjua kama 'papa fololo', jina alilopewa na rafikiye kutoka nchi ya Demokrasia ya Kongo. |
Yeye hufanya muziki wake katika mtindo unaojulikana kama kapungala ambalo anadai ni mchanganyiko wa kapuka na lingala. |
Jina lake lilijulikana kote nchini alipotoa wimbo 'system ya kapungala' wimbo aliofanya akishirikiana na Dak Eddy kutoka Eldoret. |
Daddy Owen ambaye kwa sasa ana umri wa takribani miaka 33 anasema kuwa aligundua kipaji chake katika muziki akiwa katika shule ya sekondari. Wakati huu ndipo alishighulika sana na klabu ya kuigiza na muziki. |
Shauku yake ya muziki ilikuwa juu sana wakati huu, ndiposa akatumia fulsa hii kutunga nyimbo. |
Haikuchukua muda mrefu kwa jujitoza kwake katika uwanja wa muziki baada ya kumaliza masomo ya sekondari. |
Ilikuwa mwaka wa 2003 alipoanza kazi rasmi ya muziki mwenyewe. |
Bahati ilimzidi kwa vile ndugu yake Roughtone alikuwa tayari katika sekta hii hivyo kumwekea msingi na kumwongoza katika uchanga wake katika mambo ya muziki. |
Licha ya kukumbana na changamoto ambazo ni za kawaida kwa kila msanii, Daddy Owen amejikakamua na anafanya vizuri zaidi. |
Amepokea tuzo kadhaa mojawapo ikiwa tuzo bora zaidi ya Anglophone katika tuzo ya muziki ya MTV Africa mwaka 2001. |
Alituzwa tuzo hii kwa wimbo wa 'tobina'. |
Yeye pekee ndiye mwanamuziki wa nyimbo za injili kote Afrika kupata tuzo hili. |
Baadhi ya nyimbo zake zenye umaarufu ni kama 'system ya kapungala', 'tobina', 'saluti' na 'Mbona'. |
Comments
Hide