Ken wa Maria |
Ken wa Maria anafanya muziki wake katika lugha ya kikamba. |
kwa sasa yeye ndiye msanii mmaarufu kutoka eneo la ukambani. |
Nyimbo zake ni za mtindo wa 'benga'. |
Ken anaalbamu kadhaa na zote kwa lugha ya kikamba. |
Chakushangaza ni kuwa nyimbo zake zinaumaarufu kwa watu wa maeneo yote nchini hata wasioelewa kikamba. |
Majina yake kamili ni Ken Wambua Nguze. |
Yeye anapenda kujitambulisha kama mfalme wa nyimbo za kikamba na kila mmoja aliyehudhuria tamasha zake unauhakika wa jambo hili. |
Ken huongoza bendi maarufu inayojulikana kama 'Yatta Orchestra International Band.' |
Tofauti na wanamuziki wengi waofanya muziki pekee, Ken ni mwanasiasa na mjasiriamali anayehusika hasa na nyumba za kukodisha. |
Kama mjasiriamali, Ken amelipa shilingi milioni 3 kwa nyumba katika sehemu ya Doonholm, Nairobi; anamiliki maduka matatu ya nguo mjini , pia ni mshirika katika Kinga Motors Umoja, kampuni inayohusika na magari yaliyotumika. |
Yeye ni mmojawapo ya watu wanaomiliki kampuni ya Sunset Safaris - Pur jijini Mombasa. |
Azimio la Ken wa Maria kuwania kiti cha ubunge lilikatika alipopokea vitisho vya kuuliwa kutoka kwa wanaodhaniwa kuwa wapinzani wake. |
Hivyo basi, aliamua kumuunga mkono kiongozi wake katika siasa mheshimiwa Kalonzo Musyoka aliyekuwa mgombea mwenza Mheshimiwa Raila Odinga ambaye ni kiongozi wa chama cha muungano wa CORD. |
Ken ambaye sasa anaumri wa miaka 36 ana mke na watoto wawili. |
Licha ya muziki wake kupata soko kubwa mandarini, Ken hajawai onekana katika vyombo vya habari wala kujulikana kama mwana mziki aliyesifika sana lakini mambo haya hayamtishi moyo. |
Katika mwaka wa 2001 Ken aliteuliwa kama mmoja wa waliokuwa wakigombea taji la East Africa Music Awards katika jamii ya nyimbo za mtindo wa kilingala. |
Kulingana na yeye kuteuliwa kwake ni jambo la kutosha la kuonyesha kuwa muziki wake unafanya vizuri hata kama hajaweza kupata tuzo hilo. |
Comments
Hide