Dialogue

Vocabulary (Review)

Learn New Words FAST with this Lesson’s Vocab Review List

Get this lesson’s key vocab, their translations and pronunciations. Sign up for your Free Lifetime Account Now and get 7 Days of Premium Access including this feature.

Or sign up using Facebook
Already a Member?

Lesson Notes

Unlock In-Depth Explanations & Exclusive Takeaways with Printable Lesson Notes

Unlock Lesson Notes and Transcripts for every single lesson. Sign Up for a Free Lifetime Account and Get 7 Days of Premium Access.

Or sign up using Facebook
Already a Member?

Lesson Transcript

MiambaYa Kit Mikayi.
Nina shaka kuwa umekizuru kisiwa cha ndere kinachopatikana kando ya mwamba wa ziwa victoria kaskazini mwa mji wa Kisumu ambapo mawe maarufu ya kit mikayi inapatikana. Hebu nikuambie machache kuhusu mawe haya na nina uhakika hapa ndipo mahali utapanga kuzuru katika likizo . Kit mikayi ni mwamba mkubwa ulioko kando ya barabara ya Kisumu ukielekea Bondo katika magharibi ya Kenya takribani kilomita 29 upande wa magharibi wa mji wa Kisumu. Mwamba huu una urefu wa mita sabini na kuna uwezekano kuwa hii ndiyo sehemu iliyoinuka zaidi katika eneo hili. Kuna mambo mengi ya kuvutia katika eneo hili ambayo ni pamoja na kisiwa cha Ndere na wanyama pori kama vile kiboko, mamba wa aina ya nile na Paa. Watu wengi hupendelea kukwea mwamba huu wa mikai.Unapoendelea kupanda kuna wepesi fulani ambao mtu huhisi kwa kichwa na watu wengi hudhani kuwa ni hofu ya urefu.Hii inasemekana kusababishwa na mvuto unaotaka kukurudisha nyuma mahali ulipotoka unapong'ang'ana kupanda. Watu wenye uzoefu wa kukwea milima watafurahia mvuto huo sana.Unapofikia kilele cha mwamba huu utaona mazingira ya kuvutia katika eneo hili likiwemo ziwa victoria na haya yatafanya usahau uchungu uliopitia ulipokuwa ukikwea. Lazima uwe unashangaa jinsi mwamba huu ulipata jina lake. Hadithi husimuliwa ya mzee mmoja ambaye alikuwa mpenzi wa mwamba huu kupindukia. Kila alipoamka,alienda kukaa ndani ya mwamba huu na hapo ndipo mkewe alimpekelea mamkuli yake yote . Kila alipoulizwa mkewe alikokuwa mmewe,alisema yuko katika chumba cha mkewe wa kwanza yaani mikayi akiashiria ule mwamba na hapo ndipo huu mwamba ulipata jina la kit mikayi.

Comments

Hide