John De Mathew |
John Ng'ang'a ambaye anajulikana kwa mashabiki wake kama John De Mathew alizaliwa na kupata masomo yake katika mkoa wa kati,nchini Kenya. |
Yeye ni mwimbaji maarufu kwa kabila ya wakikuyu na pia muigizaji wa bendi iliyo tambulika kwa vilabu vingi. |
Muziki wake ni wa kuburudisha na wa kupasha ujumbe. |
Midundo katika miziki yake ni ya kuvutia. |
John ni mshairi wa kipekee kama inavyoonekana katika utungaji wake wa kuunganisha maadili ya jamii na mifumo. |
Yeye hutumia methali kuelemisha jamii kwa urahisi. |
Alianza kazi ya uwimbaji akiwa kijana huku akiongozwa na kutiwa changa moto na mwimbaji mkuu wa enzi hiyo, Bwana Kamaru wa jamii ya wakikuyu. |
Alifuata nyayo zake hadi alipoweza kujimudu. |
Msanii huyu maarufu wa jamii ya wakikuyu alishtakiwa dhidi ya misemo ya chuki. |
Kamati kuu ya mshikamano na ushirikiano ilialamisha moja ya wimbo wake kama msemo wa chuki na hivi sasa anachunguzwa. |
Kabla ya hatua yoyote kuchukuliwa, ilibidi wimbo wake upitishwe kwa mtafsiri aliyeithinishwa ili kuhakikisha ubayana. |
Wimbo uliokuwa ukifanyiwa uchunguzi ni 'mwaka wa fisi'. |
Ilisemekana kuwa wimbo huu ulikua unamtania mheshimiwa Raila Odinga aliyekuwa anawania kiti cha urais katika uchaguzi uliopita. |
Wimbo huu ulipigwa marufuku na ulifaa usipeperushwe hata kidogo kwa stesheni yoyote ya redio. |
Tume ya vyombo vya habari pamoja na NCIC waliweka mikakati kuchunguza stesheni zote zinazocheza wimbo wake ili kuchukuliwa hatua kali. |
Pia, inadaiwa kuwa aliwahi kuwa na uhusiano na mwakilishi mmoja wa akinamama kutoka mkoa wa kati na kupata mtoto naye. |
Anaamini kuwa muziki unapaswa kuzingatia matukio kamili maishani na yanayonufaisha jamii kwa ujumla. |
Comments
Hide