AVRIL |
Judith Nyambura Mwangi ama Avril alizaliwa tarehe 30 mwezi wa Aprili mwaka wa 1986 mjini Nakuru, nchini Kenya. |
Alifanya masomo ya sekondari nchini Kenya na kisha kuendelea na kidato cha tano na sita nchini Uganda. |
Sasa ana shahada katika somo la kubuni bidhaa kutoka chuo kikuu cha Nairobi. |
Amesaini na kampuni ya kurekodi inayo julikana kama Ogopa Deejays na ameweza kufanya kazi na wasanii wanao tambulika humu nchini Kenya na Afrika Mashariki. |
Maisha ya Avril kama mwimbaji ulianza alipokua msichana mdogo. |
Baadaye aliweza kuwa spika wa umma ambapo aliweza kuwa mchanaji katika sherehe za shule na akaendelea na mtindo huu hadi vidato vikuu shuleni. |
Wakati huu alipokuwa shuleni, kiwanda cha muziki nchini Kenya kilikuwa changa. |
Lakini kizazi cha kwanza cha wasanii wa Pop kutoka Ogopa Deejays (ambapo yuko hata sasa) walipokuchukua hatua mpya, Avril alihisi ubora wao na maramoja kujiunga nao. |
Wakati huo ndipo aligundua kuwa alifaa kuwa mmoja wao. |
Sauti yake ya kubuni huunda hisia kubwa ambazo zinaweza kuhusishwa kwa urahisi na vijana na pia wazee duniani kote kwa ajili ya uwezo wake wa kuunganisha miundo kadhaa ya muziki. |
Hata hivyo, mwimbaji huyu aliuunda habari wakati picha zilizoonyesha uchi wake ziliweza kubandikwa na kutandazwa katika mtandao wa intaneti. |
Inaaminika kuwa alizibandika picha hizi ili apate umaarufu kwa vile hakuwa nao kama alivyonao leo. |
Aliyakanusha madai haya akidai kuwa hawezi kulifanya jambo kama hilo na kwamba picha hizo zilikuwa zimefanyiwa ukarabati na jamaa waliokuwa wanamwonea kijicho kwa kufaulu kwake. |
Wakati huu alikuwa anamwona kisiri mchezaji santuri mmoja aliyekuwa tayari na uhusiano na mchumba wake. |
Haya tuyaweke kando, aliuandika wimbo spesheli baaada ya vita vya uchaguzi nchini Kenya, ikiwa na lengo ya kuwaunganisha wakenya. |
Hamu yake ni kua Kenya itaweza kukumbatia tofauti zake katika nyanja za ukabila na kufanya kazi kwa umoja. |
Comments
Hide