UKOO FLANI MAU MAU |
Kalamashaka ni kikundi cha hiphop ambacho kinapatikana katika makaazi duni ya Dandora, Nairobi, nchini Kenya. |
Kikundi hiki kiliundwa na Johnny, Kama, na Oteraw mnamo wa miaka ya kati ya tisaini. |
Kikundi hiki kimewasaidia vijana wa Dandora kwa kuaanzisha kazi katika muziki wa kufoka. |
Pia waliunda kikundi cha Ukoo Flani Mau Mau , ambacho ni mkusanyiko wa wasanii 24 kutoka Mombasa, Nairobi na watu kadhaa kutoka Tanzania. |
Kuongezea, wameheshimika kwa sababu ya kuwainulia pazia wasanii kutoka nchi za ngambo ambao hukuja kututumbuiza humu nchini kama Lost Boyz na Coolio. |
Pia wameimba pamoja na kikundi cha Dead Prez na wanamuziki wengine wa kimataifa. |
Ukoo Flani ilitengenezea njia nyimbo za Kiswahili za kufoka na hiphop na kuzifanya kuwa na muundo mpya nchini. |
Kikundi hiki kinaumaarufu kwa wafuasi wake wa kufoka kwa ajili ya ujumbe wao unaozingatia siasa na jamii. |
Katika mwaka wa 2001, walitoa rekodi yao ya kwanza na wimbo 'Ni Wakati', ambao ulivuma sana nakutengenezea njia nyimbo, 'Fanya Mambo' and 'Tafsiri Hii' ambazo zilikuwa maarufu zaidi na kuwafanya wajulikane kiasi. |
Wamefanya maonyesho katika nchi nyingi kama Afrika Kusini, Usudi, Norwei, Uholanzi na Nigeria mwiongoni mwa nchini nyingine. |
Wana hali ya kipekee, ladha na nguvu inayotokana na makao yao ya kipekee inayowaunganisha pamoja na ujumbe chini ya kipaji cha hiphop. |
Hata hivyo, umaarufu wao ulianza kudidimia kutokana na kuibuka kwa kikundi cha genge na kapuka ambayo ingesakatwa kwa urahisi na vijana ambao asilimia yao kubwa huipenda badala ya miziki ya falsafa. |
Stesheni za redio pia zimepunguza kucheza miziki ambayo yana maadili ya kijamii kama ilivyo kawaida ya Ukoo Flani. |
Jambo hili lilichangia sana kupunguka kwa umaaarufu wa Ukoo Flani. |
Hata hivyo, wamebaki wima na kukataa kubadilika na wakati ili kufanya miziki ya kibiashara. |
Comments
Hide