Dialogue

Vocabulary (Review)

Learn New Words FAST with this Lesson’s Vocab Review List

Get this lesson’s key vocab, their translations and pronunciations. Sign up for your Free Lifetime Account Now and get 7 Days of Premium Access including this feature.

Or sign up using Facebook
Already a Member?

Lesson Notes

Unlock In-Depth Explanations & Exclusive Takeaways with Printable Lesson Notes

Unlock Lesson Notes and Transcripts for every single lesson. Sign Up for a Free Lifetime Account and Get 7 Days of Premium Access.

Or sign up using Facebook
Already a Member?

Lesson Transcript

Mbuga la wanyama la Maasai Mara
Mbuga la wanyama la Masaai Mara liko katika mkoa mkuu wa bonde la ufa, kaunti ya Narok nchini Kenya. Unaupana wa kilomita za mraba 1500. Mbuga hili ni sehemu ya mfumo wa ikolojia kubwa wa Mara, ambamo mna ranchi zifuatazo - Koiyaki, Lemek, Ol Chorro Oirowua, Olkinyei, Siana, Maji Moto, Naikara, Derkesi Ol, Kerinkani, Oloirien, na Kimintet. Mbuga hili hupakana na mbuga la Serengeti upande wa kusini, genge Siria upande wa magharibi, na maeneo ya ufugaji wa jamii ya wamaasai pande za kaskazini, mashariki na magharibi. Talek na Mara ni mito mikubwa ambayo huleta unyevu katika mbuga hili. Katika mbuga hili, kuna aina ya spishi 95 ya wanyama na zaidi ya aina 400 za ndege kumbukumbu. Mnyama pori ndio spishi kubwa kwa mbuga hili na huhama katika mwezi wa Julai na hurudi mwezi wa Novemba. Wao huhama pamoja na paa Thompsons, pundamilia na wanyama wengine wanaokula majani kutoka Serengeti nchini Tanzania na kuelekea kaskazini kwa ajili ya malisho safi. Ni vigumu mgeni kuwakosa wanyama wakubwa watano ambao ni; nyati, tembo, chui, simba na kifaru katika hili mbuga. Wanyama wengine ni pamoja na; Viboko, Duma, swala, Paa, kongoni, twiga na popo mbweha. Katika mbuga hili, idadi ya vifaru weusi walikuwa juu mpaka mwaka wa 1960. Baada ya hapo, idadi hii ilipungua sana kutokana na ujangili katika miaka ya 1970 na miaka ya mwanzo ya 1980. Hata hivyo, idadi hii inaongezeka kwa vile ujangili umepungua na kukomeshwa. Katika mito Mara na Teleki, mamba na viboko wa mto Nile hupatikana kwa idadi kubwa. Aidha, mbuga la wanyama la Masaai Mara ni kituo cha utafiti wa fisi mwenye madoadoa.

Comments

Hide