Kuja kuzaliwa |
Hiki kitabu cha kuvutia kimeandikwa na Marjorie Oludhe Macgoye mzaliwa wa uingereza ambaye amekuwa mkazi wa nchi ya Kenya kwa muda mrefu. |
Wahusika wakuu katika hii hadithi ni Martin na mkewe Paulina ambao wamefunga ndoa hivi karibuni. |
Katika mwanzo wa hadithi, Paulina ambaye ana umri wa miaka 16 ni mjamzito. |
Anasafiri kutoka kijijini hadi mji mkuu wa Nairobi kujiunga na mumewe anayeishi na kufanya kazi Kariokor. |
Inatokea kwamba baada ya siku chache, Paulina anakuwa mgonjwa na kupelekwa katika hospitali ya pumwani. |
Kwa bahati mbaya ile mimba inatoka. |
Analazwa hospitalini lakini siku ya pili anaamua kutoka na kuelekea nyumbani bila kumngojea mumewe. |
Kwa bahati mbaya anapotea njia na kwasababu hafanikiwi kufika nyumbani, inamlazimu aishi nje kwa siku mbili. |
Hatimaye, Martin anampata lakini amekasirika kwavile Paulina hakumngojea. |
Usiku huo na kwa mara ya kwanza anamchapa bibiye. |
Hadithi hii inaendelea na Paulina anapata mimba zingine lakini zote zinatoka kabla ya wakati wa kujifungua. |
Ndoa yao inazidi kuwa ngumu, na kutofautiana pia kunaongezeka. |
Martin anaanza kutokuwa mwaminifu na kuanza uhusiano na wanawake wengine. |
Paulina naye anaamua kumuacha na kuelekea Kisumu. |
Huko anafanikiwa kupata kazi ya uwalimu. |
Naye pia anabadilisha mienendo na kuanza kuhusishana na mwanaume mwingine. |
Chakushangaza ni kuwa wakati huu anafanikiwa kujifungua mtoto wa kiume. |
Furaha yake inakatizwa wakati mtoto huyu anauliwa na polisi wanapofyatulia umati risasi katika mji wa Kisumu. |
Paulina anaamua kurudi Nairobi ambapo anaajiriwa kama mjakazi kwa tajiri mmoja ambaye yuko katika harakati za siasa. |
Martin anaanza kumtembelea Paulina na wakati kitabu hiki kinamalizika wameshakuwa mume na mke tena. |
Mara hii, Paulina anafanikiwa kumpa Martin mtoto. |
Comments
Hide