SIKU NJEMA |
Hii ni hadithi iliyoandikwa na mwandishi anayejulika sana kwa uadishi wa riwaya wa lugha ya kiswahili. |
Anajulikana kama Ken Walibora. |
Mhusika mkuu katika riwaya hii ni Msanifu Kombo ambaye baadaye alipata jina Kongowea Mswahili baada ya kushinda tuzo katika mashindano ya utunzi. |
Mazingira ya hadithi ni Tanga nchi Tanzania. |
Kombo anakabiliwa na matatizo mengi maana alikuwa na mzazi mmoja tu, mamake Zainabu Makame. |
Bi.Makame alikuwa mwimbaji wa muziki wa kitaarab, maarufu nchini Tanzania na katika mkoa wa pwani wa Kenya. |
Kutokuwa na baba mzazi kwa Kombo kulivutia ubaguzi mwingi hasa kutoka kwa wanafunzi wenzake shuleni. |
Kitamaduni, kutokuwa na baba mzazi unayemjua ilikuwa jambo lisilokubalika. |
Mambo yalizidi kuwa magumu kwa Kombo baada ya mamake kufa. |
Alilelewa na shangazi yake na mama wa kambo ambao walimdhulumu sana. |
Ubanguzi shuleni na dhuluma nyumbani ulifanya maisha yake kuwa magumu. |
Licha ya hayo yote yeye ni mwandishi mwenye kipaji. |
Ni jambo hili alilotumia kuwashinda wenzake na kumfanya mwanafunzi mwenye umaarufu shuleni. |
Baadaye, aliamua kutorokea nchini Kenya kumtafuta babake mzazi ambaye alikuwa amemwona kwa picha tu. |
Juhudi zake hazikuwa za bure kwa kuwa mwishowe aliweza kumpata. |
Babake alikuwa mshairi maarufu aliyejulikana kama Juma Mkosi. |
Hata hivyo watu wengi walimjua kwa jina lake la ushairi Amju Aiskom ambalo ni endelezo la jina lake likiwa limeanziwa kutoka nyuma. |
Wakati hadithi hii inafikia mwisho, siku njema inamjia Kongowea kwa ajili ya kumpata babake mzazi na kwa wakati huu ameshaoa Vumilia Binti Abdulla. |
Anaendelea na hamu ya kuandika kwani anaonekana kana kwamba amekuwa akiandika kitabu hiki usiki mzima. |
Kitabu hiki kinadhaniwa kinamhusu bibiye anayetokezea kwa nyuma na kumkumbatia, hapo ndipo linamdua kuwa jua limeshachomoza. |
Comments
Hide