Dialogue

Vocabulary (Review)

Learn New Words FAST with this Lesson’s Vocab Review List

Get this lesson’s key vocab, their translations and pronunciations. Sign up for your Free Lifetime Account Now and get 7 Days of Premium Access including this feature.

Or sign up using Facebook
Already a Member?

Lesson Notes

Unlock In-Depth Explanations & Exclusive Takeaways with Printable Lesson Notes

Unlock Lesson Notes and Transcripts for every single lesson. Sign Up for a Free Lifetime Account and Get 7 Days of Premium Access.

Or sign up using Facebook
Already a Member?

Lesson Transcript

SIKU NJEMA
Hii ni hadithi iliyoandikwa na mwandishi anayejulika sana kwa uadishi wa riwaya wa lugha ya kiswahili.
Anajulikana kama Ken Walibora.
Mhusika mkuu katika riwaya hii ni Msanifu Kombo ambaye baadaye alipata jina Kongowea Mswahili baada ya kushinda tuzo katika mashindano ya utunzi.
Mazingira ya hadithi ni Tanga nchi Tanzania.
Kombo anakabiliwa na matatizo mengi maana alikuwa na mzazi mmoja tu, mamake Zainabu Makame.
Bi.Makame alikuwa mwimbaji wa muziki wa kitaarab, maarufu nchini Tanzania na katika mkoa wa pwani wa Kenya.
Kutokuwa na baba mzazi kwa Kombo kulivutia ubaguzi mwingi hasa kutoka kwa wanafunzi wenzake shuleni.
Kitamaduni, kutokuwa na baba mzazi unayemjua ilikuwa jambo lisilokubalika.
Mambo yalizidi kuwa magumu kwa Kombo baada ya mamake kufa.
Alilelewa na shangazi yake na mama wa kambo ambao walimdhulumu sana.
Ubanguzi shuleni na dhuluma nyumbani ulifanya maisha yake kuwa magumu.
Licha ya hayo yote yeye ni mwandishi mwenye kipaji.
Ni jambo hili alilotumia kuwashinda wenzake na kumfanya mwanafunzi mwenye umaarufu shuleni.
Baadaye, aliamua kutorokea nchini Kenya kumtafuta babake mzazi ambaye alikuwa amemwona kwa picha tu.
Juhudi zake hazikuwa za bure kwa kuwa mwishowe aliweza kumpata.
Babake alikuwa mshairi maarufu aliyejulikana kama Juma Mkosi.
Hata hivyo watu wengi walimjua kwa jina lake la ushairi Amju Aiskom ambalo ni endelezo la jina lake likiwa limeanziwa kutoka nyuma.
Wakati hadithi hii inafikia mwisho, siku njema inamjia Kongowea kwa ajili ya kumpata babake mzazi na kwa wakati huu ameshaoa Vumilia Binti Abdulla.
Anaendelea na hamu ya kuandika kwani anaonekana kana kwamba amekuwa akiandika kitabu hiki usiki mzima.
Kitabu hiki kinadhaniwa kinamhusu bibiye anayetokezea kwa nyuma na kumkumbatia, hapo ndipo linamdua kuwa jua limeshachomoza.

Comments

Hide