Hamjamboni, mimi ni Medina. |
Sikukuu ya mwaka mpya inasherehekewa mnamo tarehe 1 January kila mwaka. Hii ni siku ambayo watu wengi hutazama maisha yao ya mwaka uliopita na kutaka kubadilisha maazimio yao na kuwa na mtazamo mpya wa maisha. |
Funzo hili, litatuangazia jinsi watu hujiburudisha pamoja na jamaa na marafiki. |
Je, ni wakati upi ambao watu wengi hupata muda wa kubadilisha mielekeo ya maisha yao? Ni wakati ngani wa mwaka wazazi wengi |
huwanunulia watoto wao zawadi mpya? |
Tutawaonyesha jibu la swali hili mwishoni mwa video hii. Watu hungoja sikukuu ya mwaka mpya kwa shauku kuu. Waamini huenda kanisani na kukesha huko huku wakigonja saa sita ya usiku kuwasili. Watu wengine huona heri kuenda kwa makao ya burudani na kujistarehesha kwa kuimba na kupiga muziki. Saa sita ya usiku ikifika wao hupiga nduru, kurusha miale ya moto na kuukaribisha mwaka mpya kwa hoi hoi na nderemo. Watu hutuma ujumbe mfupi kwa jamaa na marafiki na kuukaribisha mwaka mpya. Walio katika mahali pa ibada huomba na kumshukuru mungu. |
Asubuhi ifikapo watu huanza kutayarisha mlo wa kipekee pamoja na vinywaji. Wao huwaalika wageni na kuwapa burudani murua kabisa. Watu wengi hupendelea kuchinja mbuzi na kupika chakula kama chapati, mukimo, pilau na vitoweo vya aina mbali mbali. Vinywaji pia hupatikana kwa wingi. Nazo ni kama: soda, maji ya matunda, pombe na vileo tofauti. |
Masaa ya alasiri watu wanapomaliza kula na kunywa wao huvalia mavazi mapya yanayopendeza na kuenda mahala pa kujistarehesha. Kwa mfano wanaweza kuenda kuona wanyama wa pori ama kuogelea huko pwani. Sikukuu kama hii hufanya utalii wa kinyumbani kufana sana. |
Siku hii watu hufanya matendo ya kutia fora kwa sababu wanaimani ya kwamba wakiwa wazuri mwanzoni mwaka wao utakuwa wenye fanaka. Wao huanza na nia mpya. |
Na sasa nitawapa jibu la swali la hapo awali. |
Je, ni wakati upi ambao watu wengi hupata muda wa kubadilisha mielekeo wa maisha yao? Ni wakati upi wa mwaka wazazi wengi huwanunulia watoto wao zawadi mpya? |
Watu wengi huchukulia sikukuu hii kama wakati wa kuanza mienendo mapya. Wazazi pia hutaka kuwafurahisha wanao na wawapendao kwa zawadi tofauti. |
Funzo hili lilikuwaje? Je, ulijiifunza jambo lolote la kusisimua? |
Je nyinyi husherehekea sikukuu ya mwaka mpya kama Wakenya? |
Tuwachie maoni yako katika SwahiliPod101.com kisha tuonane katika somo lifuatalo! |
Comments
Hide