Dialogue

Vocabulary (Review)

Learn New Words FAST with this Lesson’s Vocab Review List

Get this lesson’s key vocab, their translations and pronunciations. Sign up for your Free Lifetime Account Now and get 7 Days of Premium Access including this feature.

Or sign up using Facebook
Already a Member?

Lesson Transcript

Hamjamboni, mimi ni Medina.
Sikukuu ya Madaraka inasherehekewa na wakenya kama ukumbusho wa wakati ambao nchi yao ilipata madaraka mnamo wa mwaka wa 1963 kutoka kwa waingereza. Inasherehekewa tarehe 1 mwezi wa sita kila mwaka.
Funzo hili linatoa elimu kuhusu jinsi wakenya husherehekea ukumbusho wa kujitawala wenyewe kama nchi.
Je, unajua Sikukuu ya Madaraka ni sikukuu inayosherehekewa hata nje ya mipaka ya Kenya?
Tutawaonyesha jibu la swali hili mwishoni mwa video hii.
Katika sherehe hii, tukio la kwanza linahusisha maonyesho ya burudani ya kitamaduni. Nyimbo za kale huchezwa kutoka sehemu tofauti za nchi. Nyimbo zinazoashiria kupenda nchi hutumbuiza wageni waheshimiwa wa serikali na pia raia wa kawaida ambao hujitokeza kwa wingi katika uwanja wa kitaifa wa Nyayo ambako sherehe hizi hufanyika.
Wanajeshi wa vitengo mbali mbali hufanya maonyesho yao na kuwatumbuiza waliohudhuria. Wanajeshi wa maji, wa nchi kavu na wale wa hewani huwa wameandaa maonyesho maalum kwa kutumia vifaa vyao vya muziki. Rais wa taifa hukagua walinda jeshi wa heshima na hutoa hotuba ambayo hungojewa sana kama ilivyokuwa desturi ya sikukuu zote za kitaifa. Wale ambao hawawezi kuhudhuria sherehe hizi katika uwanja wa Nyayo hutazama sherehe hii kwa runinga au kusoma kutoka kwa magazeti siku ifuatayo.
Baadaye watu hupenda kujistarehesha kivyao. Watu wa jamaa moja wanaweza amua kuenda kwa mandari na kufurahia michezo katika viwanja vya umma. Wengine huamua kusafiri hadi mashambani na kuchinja mbuzi na kuku kwa vile wakenya hupenda nyama. Katika mji wa Nairobi na miji mingine mikubwa, biashara huzorota lakini biashara katika sekta ya usafiri hasa ya kwenda mashambani hunoga sana.
Ni katika sikukuu hii ndio Wakenya walipata kujitawala lakini walingojea kwa miezi sita kabla ya kutangazwa kama nchi huru. Sikukuu ya Jamhuri ambayo inasherehekewa tarehe 12 Decemba ndio siku ambayo Kenya ilipata utawala kamili.
Na sasa nitawapa jibu la swali la hapo awali.
Je, unajua Sikukuu ya Madaraka ni sikukuu inayosherehekewa hata nje ya mipaka ya Kenya?
Sikukuu ya Madaraka ni sikukuu rasmi ya kitaifa ambayo husherehekewa na watu wote wapendao nchi yao ya Kenya, ikiwamo watu walio ng`ambo kwa ajili ya masomo ama kazi. Ni siku ambayo Wakenya walichukua utawala kutoka kwa mabeberu na kupata kujitawala.
Funzo hili lilikuwaje? Je, ulijiifunza jambo lolote la kusisimua?
Je, nchi yenyu ilitawaliwa na mabeberu? na kama ni ndio, mabeberu walitoka nchi gani?
Tuwachie maoni yako katika SwahiliPod101.com kisha tuonane katika somo lifuatalo!

Comments

Hide