Dialogue

Vocabulary (Review)

Learn New Words FAST with this Lesson’s Vocab Review List

Get this lesson’s key vocab, their translations and pronunciations. Sign up for your Free Lifetime Account Now and get 7 Days of Premium Access including this feature.

Or sign up using Facebook
Already a Member?

Lesson Transcript

Hamjamboni, mimi ni Medina.
Sikukuu ya mashujaa husherehekewa mnamo wa tarehe 20 mwezi wa kumi wa kila mwaka. Inasaidia kuwakumbuka na kuwafurahia mashujaa ambao walipigana na mabeberu hadi Kenya ikapata utawala wa kibinafsi.
Fundisho hili linatoa elimu kuhusu matukio yanayofanyika katika sikukuu hii.
Je, unajua kama sikukuu hii ilikuwa na jina lingine hapo awali?
Tutawaonyesha jibu la swali hili mwishoni mwa video hii.
Sikukuu ya Mashujaa huandaliwa katika Uwanja wa Kitaifa wa Nyayo na pia katika makao makuu ya majimbo. Pia, walio nje ya nchi kwa shughuli mbali mbali huandaa sherehe hizi ambazo huhudhuriwa na mabalozi wa Kenya katika nchi hizo. Katika Uwanja wa Nyayo, Rais wa nchi hupokelewa na mkuu wa majeshi na baadaye ibada ya dini zote hufanyika. Maombi hufanywa na askofu, imam na kasisi wa kitamaduni.
Wakongwe wa MAU MAU ambao ni kikundi kilichong'ang'ania uhuru pia hualikwa na serikali. Kama ilivyo desturi ya sikukuu zote rasmi za serikali, Rais hutoa hotuba yake na kuongea kuhusu shida zilizoko na pia jinsi Kenya itasonga mbele kwa amani. Raia wengi huenda katika Uwanja wa Kitaifa wa Nyayo. Wengine huona maonyesho hayo kwa runinga.
Baada ya sherehe hizi kutia nanga masaa ya adhuhuri, watu hupumzika na kujistarehesha na vinywaji na nyama choma ambayo ni chakula kipenzi kwa wakenya wengi. Watu hupendelea kukutana na waandani na jamaa zao manyumbani ama huko nje kwa mikahawa na kwa mandari.
Kwa vile wafanyakazi hawaendi kazini na wanafunzi hawaendi shuleni, watu wengi hulala usiku sana na kuamka baada ya macheo kwa vie walilala fo fo fo kwa usingizi mnono.
Na sasa nitawapa jibu la swali la hapo awali.
Je, unajua kama sikukuu hii ilikuwa na jina lingine hapo awali?
Sikukuu hii ilikuwa inaitwa Sikukuu ya Kenyatta kabla ya katiba mpya kuzinduliwa mwaka wa 2010. Ilikuwa kama ukumbusho wa mashujaa sita akiwemo Jomo Kenyatta waliozuiliwa huko Kapenguria. Sasa inasherehekea mashujaa wote sita na wengineo walio saidia uhuru kupatikana.
Funzo hili lilikuwaje? Je, ulijiifunza jambo lolote la kusisimua?
Je, kuna mashujaa wowote waliosaidia serikali ya nchi yako na walisaidiaje?
Tuwachie maoni yako katika SwahiliPod101.com kisha tuonane katika somo lifuatalo!

Comments

Hide