Hamjamboni, mimi ni Medina. |
Sikukuu ya ukumbusho wa kuchukuliwa mbinguni kwa bikira Mariamu inasherehekewa mnamo tarehe 15 Agosti. Waumini wa kanisa ya kikatoliki kote duniani na pia nchini Kenya huitambua sana. |
Fundisho hili litatoa elimu kuhusu jinsi wakristo wakatoliki husherehekea Jumapili hii. |
Je, unafahamu ni baba mtakatifu mgani aliyetangaza sikukuu hii na ilikuwa enzi ipi? |
Tutawaonyesha jibu la swali hili mwishoni mwa video hii. |
Waumini huamka mapema na kufanya maandamano ya kufana kwa njia za miji na hutumia miale ya moto kusherehekea sikukuu hii. Muundo wa bikira Mariamu hubebwa hadi pahala pateule ambapo pamepangwa maua ya sherehe na ambapo pana muundo wa Yesu Kristo ambaye humngoja. |
Miundo yote miwili huwekwa pamoja mara tatu. Muundo wa Yesu Kristo huutangulia wa bikira Mariamu katika shughuli ya kurudi kule kanisani kwa ibada maalum ya Baraka. Maombi ya kusisitiza imani ya kwamba mwili wa bikira Mariamu uliinuka juu mbinguni na kuungana na roho yake hufanyika. Waumini huomba bikira Mariamu awaombee na kuwatetea kwa mungu kama mama wa Yesu Kristo. |
Kule kanisani ibada maalum ya baraka hufanyika na maji mawaridi hunyunyusiwa waumini kama ishara ya baraka. Waumini huimba nyimbo na kutumbuiza wenzao kwa nyimbo na usanii huku wamevalia nguo za kuiga wanaume watatu wajanja ambao wameongelewa katika bibilia takatifu. |
Sikukuu hii haikuwa desturi ya kanisa ya kikatoliki ya Roma hadi 1950. Imani hii pia inadumishwa na wakristo halisi pamoja na wa kianglikana na wengineo. Bikira Mariamu huonekana kwa jua miguu yake ikiwa juu ya mwezi. |
Na sasa nitawapa jibu la swali la hapo awali. |
Je, unafahamu ya kuwa sikukuu hii ilitangazwa na baba mtakatifu mgani na ni enzi ipi? |
Sikukuu ya kuchukuliwa mbinguni kwa bikira Mariamu ilianza kusherehekewa enzi ya 1950 wakati baba mtakatifu wa Rumi Pius XII alipotangaza iwe sikukuu. |
Funzo hili lilikuwaje? Je, ulijiifunza jambo lolote la kusisimua? |
Je, nchi yako ina waumini wowote wa kikatoliki? Kama ndio, wao husherehekea sikukuu hii kivipi? |
Tuwachie maoni yako katika SwahiliPod101.com kisha tuonane katika somo lifuatalo! |
Comments
Hide