Dialogue

Vocabulary (Review)

Learn New Words FAST with this Lesson’s Vocab Review List

Get this lesson’s key vocab, their translations and pronunciations. Sign up for your Free Lifetime Account Now and get 7 Days of Premium Access including this feature.

Or sign up using Facebook
Already a Member?

Lesson Transcript

Hamjamboni, mimi ni Medina.
Sikukuu hii ya watakatifu husherehekewa mnamo wa tarehe moja mwezi wa Novemba na wakristo kote duniani na pia nchini Kenya. Ni sherehe inayowaheshimu watakatifu na wafia dini ambao ni watu waliokataa kukana madini yao na ndiposa wakauwawa kwa ajili ya imani yao.
video hii inakusudia kutoa elimu jinsi waumini nchini Kenya husherehekea Sikukuu ya watakatifu.
Je, unajua ni wakristo wa mlengo upi ambao husherehekea sikukuu hii?
Tutawaonyesha jibu la swali hili mwishoni mwa video hii.
Nchini Kenya, wakristo huungana katika kanisa la kikatoliki la takatifu ya familia ya Basilica jijini Nairobi kwa misa ya kusherehekea watakatifu wote. Waumini huulizwa na askofu mkuu wapeane majina ya wawapendao walioaga dunia ndiposa wafanyiwe maombi. Yeye huwaombea pamoja na wafia dini wengine kote duniani.
Baadhi ya waumini huandaa mikutano ya kifamilia na kufanya ibada ambayo huongozwa na askofu kando ya makaburi ya wawapendao. Hapa, wao hustahili dini, kuimba nyimbo za dini na kuomba huku wengine wao wakikunywa vinywaji tofauti.
Kesho yake kuna tukio ya kusherehekea na kuombea roho zote za walioenda jongomeo. Siku hii huitwa "siku ya roho zote". Wahubiri, marafiki na jamaa hutembelea makaburi na kuwekelea jiwe la kaburi na maua kama mojawapo ya njia ya ukumbusho wa marehemu.
Biashara ya maua na ya tawafa huimarika sana siku ya watakatifu wote na siku ifuatayo ya kuziombea roho zote. Kwa minajili hizi za dini, maua na tawafa hutumika sana.
Na sasa nitawapa jibu la swali la hapo awali.
Je, unajua ni wakristo wa mlengo upi wa dini ambao husherehekea sikukuu hii?
Wakristo waumini wa kanisa la kikatoliki, wa kianglikana na baadhi ya wale wasiokubaliana na mafundisho ya kanisa la kirumi husherehekea sikukuu hii ya kuwaheshimu wafu wa dini.
Funzo hili lilikuwaje? Je, ulijiifunza jambo lolote la kusisimua?
Je, nchini mwenu kuna wafia dini au watakatifu? Kama ndio, kuna siku ya kipekee ya kuwakumbuka na kuwapongeza?
Tuwachie maoni yako katika SwahiliPod101.com kisha tuonane katika somo lifuatalo!

Comments

Hide