Hamjamboni, mimi ni Medina. |
Sikukuu ya Yesu Kristo ya kupaa juu ni siku ya arobaini ya pasaka. Hii inamaanisha kuwa tarehe haswa ya sikukuu hii huamuliwa kulingana na pasaka hata ingawa imesalia mnamo tarehe Mei 29 kwa muda mrefu sasa. Ni sikukuu inayosherehekewa na wakristo kama ukumbusho wa wakati Yesu alipaa kwenda mbinguni. |
Video hii itakufanya kujua jinsi wakristo husherehekea sikukuu hii |
Je, ni akina nani waliuona muujiza huu Yesu Kristo alipokuwa akipaa na kwenda mbinguni? |
Tutawaonyesha jibu la swali hili mwishoni mwa video hii. |
Wakristo wengine na haswa wakatoliki huenda kanisani siku hii ya alhamisi lakini wakristo wengine huenda kanisani jumapili ifuatayo. Kuna wale hukosa kwenda kanisani kabisa na kukaa nyumbani. Waumini huwasha mshumaa na kukariri imani yao na kuomba na kula chakula cha sherehe pamoja. |
Katika maduka na ofisi za wakristo, utapata ya kwamba mazingira ni tofauti kwavile wao hunyamaza huku waki dhamiria kukuja tena kwa Yesu Kristo. Huu ni wakati ambao waumini huwa na imani ya kwamba Yesu atawabeba na kupaa na wao mbinguni wakaishi maisha ya kusifu na furaha pamoja na mungu. |
Watu huenda nje kwa msitu ili kusikiza ndege wakiimba wakati wa macheo. Wao huamini ya kwamba wakisikia ndege wakiimba kutoka mashariki hadi magharibi hiyo ni ishara ya bahati ya mtende. Wakristo huchukua nafasi hii kuomba, kukiri dhambi na kutubu kabla ya alfajiri kufika. |
Kulingana na bibilia katika kitabu cha matendo ya mitume upaaji juu wa Yesu Kristo ulifanyika katika mlima wa Olive lakini pahala hapa kuna kanisa ambayo inatawaliwa na waislamu. |
Na sasa nitawapa jibu la swali la hapo awali. |
Je, ni akina nani waliuona muujiza huu Yesu Kristo alipokuwa akipaa na kwenda mbinguni? |
Kulingana na imani ya wakristo Yesu Kristo alikuwa akitokea kwa wafuasi wake na kuwapa mafunzo hasa baada ya kufufuka. Siku hii aliwapeleka katika mlima wa Olive na walimuona akipaa juu mbinguni. |
Funzo hili lilikuwaje? Je, ulijiifunza jambo lolote la kusisimua? |
Je, kama wakristo, watu nchini mwenu wanaamini ya kwamba kuna maisha baada ya mauti? |
Tuwachie maoni yako katika SwahiliPod101.com kisha tuonane katika somo lifuatalo! |
Comments
Hide