Hamjamboni, mimi ni Medina. |
Sikukuu ya Eid al-Adha ni sikukuu ya kiislamu ambayo husherehekewa mnamo tarehe 15 mwezi wa Oktoba kila mwaka ama siku ya kumi kwa kalenda ya kiislamu, Dhu al-Hijjah |
Fundisho hili litatoa elimu jinsi waislamu wa Kenya husherehekea sikukuu ya Eid al-Adha. |
Je, unajua ni kwa nini sikukuu hii inaitwa sikukuu ya kafara? |
Tutawaonyesha jibu la swali hili mwishoni mwa video hii. |
Waislamu huona siku ya Eid al-Adha kama fursa ya nafasi ya pili. Siku hii huja mwisho wa Hajj na waumini huajibika kwa utakaso pamoja na kujitolea. Waislamu wengi hufanya matendo ya kuiga mfano wa nabii Abrahamu na kuishi maisha ya utiifu na kujitolea mhanga kama mafundisho ya Koran inavyosema. |
Kusherehekea sikukuu hii, waislamu hununua nguo mpya na kuwatembelea marafiki na jamaa zao. Alfajiri na mapema watu hukariri Takbir ambayo ni msemo wa imani na baadaye kufanya maombi ya kijumla kabla ya macheo, Salat al-Eid. Waumini huwasalimia wenzao kwa maamkizi ya kiarabu na kuwatakia Eid yenye Baraka (Eid Mubarak). Baadaye wao hubadilishana zawadi. |
Tukio la tatu linahusisha uchinjaji wa wanyama. Walio na uwezo huchinja ngombe, mbuzi, kondoo na ngamia ama mnyama mwingine yeyote anayeliwa na binadamu. Wao hujiwekea kiasi cha nyama halafu hupeana ingine kwa jamaa, marafiki na wadhaifu kwa jamii. Watu ambao hawana uwezo wa kuchinja wanyama hununua nyama kutoka kwa duka la nyama la Halal. |
Alama kuu ya siku hii ni maombi ya asubuhi na kuchinja wanyama na kupeana nyama kwa maskini. Waislamu nchini Kenya hupenda kugawa wanyonge katika jamii kafara ili nao pia washerehekee siku hii kwa furaha. |
Na sasa nitawapa jibu la swali la hapo awali. |
Je, unajua ni kwa nini sikukuu hii inaitwa sikukuu ya kafara? |
Siku hii ni ukumbusho wa utiifu wa Abrahamu kwa Allah hasa kukubali kumtoa kafara mwanawe aliyeitwa Isaka. Abraham na Isaka walikuwa wamekubali kutolea Mungu sadaka lakini mungu mwenyewe akawasimamisha na kuwapa kondoo ili wamtolee kama sadaka. |
Funzo hili lilikuwaje? Je, ulijiifunza jambo lolote la kusisimua? |
Sikukuu hii ya kutoa kafara ina umuhimu wowote kwa nchi yako? |
Tuwachie maoni yako katika SwahiliPod101.com kisha tuonane katika somo lifuatalo! |
Comments
Hide