Dialogue

Vocabulary (Review)

Learn New Words FAST with this Lesson’s Vocab Review List

Get this lesson’s key vocab, their translations and pronunciations. Sign up for your Free Lifetime Account Now and get 7 Days of Premium Access including this feature.

Or sign up using Facebook
Already a Member?

Lesson Transcript

Hamjamboni, mimi ni Medina.
Sherehe ya sikukuu ya Mwaka Mpya ya Kiislamu huwakumbusha wafuasi wa dini wa kiislamu wakati nabii Mohammad alihama kutoka Mecca nakuelekea Medina. Wakati huu unajulikana kama mwaka wa Hegira. Waumini huswali, husoma Koran na hujirudia kwa utulivu kuhusu Hegira. Tarehe ya kusherehekea sikukuu hii huwa tofauti kila mwaka.
Fundisho hili litakufanya kujua jinsi Waislamu nchini Kenya husherehekea sikukuu hii.
Je, unajua mwezi wa kwanza wa mwaka wa kiislamu unaitwa aje?
Tutawaonyesha jibu la swali hili mwishoni mwa video hii.
Waislamu hutumiana kadi za mwaka mpya wa kiislamu nakutakiana kila la heri. Wao huenda kwa msikiti na kukariri Koran takatifu pamoja na kuswali. Ibada hii huongozwa na Imam. Mwaka mpya hungojewa kwa hamu. Watu wengine hukaa msikitini hadi usiku wa manane.
Waislamu hufunga kukula na kukunywa mchana katika siku za tisa, kumi na kumi na moja ya Muharram. Wakati huu misikiti hupeana mlo wa bure wakati wa usiku. Waislamu huungana kwa vikundi vikubwa kwa njia na kuhusika katika kufanya jambo la busara kama vile kusafisha njia za miji na kuandaa michezo kama mojawapo ya njia ya kusherehekea.
Waislamu hukusanyika pamoja na kutembea kwa mwendo wa kijeshi wakati wa usiku ili kuukaribisha mwaka mpya. Wao huimba nyimbo za kumsifu mungu wakiwa wamevalia nguo za kale. Hawana ruhusa ya kuongea, kula ama kunywa wakati wa safari yao. Kusudio lao la kutembea kwa unyamavu ni kutaka kuwatia watu moyo kwa kuswali na kumshukuru Allah kwa kuwalinda na kuwapea fanaka. Waislamu wengine hupeana sadaka ya chakula ili kushukuru mwenyezi mungu kwa mapato yao.
Sikukuu ya kiislamu ya mwaka mpya sio sikukuu ya kitaifa nchini Kenya, lakini biashara na makampuni za kiislamu zinaweza kosa kufunguliwa. Kuna uwezekano wa msukumano kwa misikiti hasa jioni na usiku.
Na sasa nitawapa jibu la swali la hapo awali.
Je, unajua mwezi wa kwanza wa mwaka wa kiislamu unaitwa aje?
Mwezi wa kwanza wa kiislamu unaitwa Muharram. Mwaka huu unamiezi kumi na mbili na siku mia tatu hamsini na nne kinyume na mwaka wa kawaida ulio na siku mia tatu sitini na nne na robo.
Funzo hili lilikuwaje? Je, ulijiifunza jambo lolote la kusisimua?
Je, kulingana na dini za nchi yako, kuna sikukuu ngapi za mwaka mpya za kidini na zisizo za kidini?
Tuwachie maoni yako katika SwahiliPod101.com kisha tuonane katika somo lifuatalo!

Comments

Hide