Hamjamboni, mimi ni Medina. |
Sikukuu ya Diwali, inayomaanisha sherehe ya mwangaza, husherehekewa kushangilia ushindi wa uzuri dhidi ya ubaya. Siku hii ambayo husherehekewa katikati ya mwezi wa Oktoba au wa Novemba inatambulika na wahindi kote duniani Kenya ikiwa moja wapo. Diwali ni sikukuu ya kitaifa nchini Kenya. |
video hii itakufanya kujua kuhusu sherehe za Diwali nchini Kenya. |
Je, uko na dokezo lolote la kuwa ni dini gani ama watu wapi ambao husherehekea Diwali? |
Tutawaonyesha jibu la swali hili mwishoni mwa video hii. |
Watu hununua bidhaa za sherehe za Diwali. Bidhaa hizi ni vyombo vya jikoni na madoido kadhaa kama vile Diwali mithai na zinginezo. Wao huvaa nguo mpya na kudumisha usafi wa hali ya juu. Wahindi pia huoka switi, kumbwe na chakula zingine kama sadaka za Dawali kama ilivyo desturi. Marafiki na jamaa hualikwa kwa chakula na baadaye wao hubadilishana zawadi, hucheza michezo tofauti na pia hucheza ngoma. |
Watu huosha nyumba zao na pahala pa kazi kwa kina. Nguo, vyumba vyote husafishwa na takataka zote hutupwa nje. Tambiko la kujitakasa hufanyika ili kutoa vitu zote zisizohitajika kwa mazingira ili kuashiria ya kuwa mtu yuko tayari kupokea miungu. Watu hufanya michoro ya miguu kwa unga wa mchele na unga mwekundu kama ishara ya kuwa miungu wamekaribishwa. |
Siku hii, watu hurembesha milango kwa nyumba zao ama biashara na mikeka ya zamani yenye rangi ya kupendeza ama michoro ya Rangoli. Usiku ifikapo, taa ndogo za mafuta huwashwa “diyas” na kuwekwa kila mahali. Taa zote za umeme na mishumaa huashwa na fataka hurushwa kwa hewa ili kufukuza ubaya kutoka kwa mazingira yako. Taa hizi huashiria kujua, au elimu inayoleta amani na kuondoa ujinga na giza maishani. |
Wakati wa sherehe za Diwali, wanawake huvalia mapambo ya dhamani kuu pamoja na Sari ama Salwar-Kurta. Wanaume nao huvaa Kurthas na kuonekana wakiwa maridadi sana. |
Na sasa nitawapa jibu la swali la hapo awali. |
Je, uko na dokezo lolote la kuwa ni dini gani ama watu wapi ambao husherehekea Diwali? |
Hata ingawa siku ya Diwali inahusishwa sana na dini ya kihindi, kuna dini zingine ambazo huitambua. Nazo ni kama Ubudha, Ujaini na Usikhi. Hata hivyo kuna waumini wachache sana wa dini za Ujaini na Usikhi. |
Funzo hili lilikuwaje? Je, ulijiifunza jambo lolote la kusisimua? |
Je, kuna wahindi nchini mwenu na kama wako, wao husherehekea sikukuu ya Diwali? |
Tuwachie maoni yako katika SwahiliPod101.com kisha tuonane katika somo lifuatalo! |
Comments
Hide