Dialogue

Vocabulary (Review)

Learn New Words FAST with this Lesson’s Vocab Review List

Get this lesson’s key vocab, their translations and pronunciations. Sign up for your Free Lifetime Account Now and get 7 Days of Premium Access including this feature.

Or sign up using Facebook
Already a Member?

Lesson Transcript

Hamjamboni, mimi ni Medina.
Sikukuu ya Lamu ya kusherehekea utamaduni ilianzishwa mwaka wa 2001 ili kushangilia urithi wa kipekee wa kiswahili wa funguvisiwa mjini Lamu. Sherehe hizi hutendeka kwa siku tatu kila mwaka lakini kila mwaka una nyakati tofauti. Hata hivyo, sherehe hizi hufanyika sana sana mwezi wa Oktoba na Novemba.
Kupitia funzo hili utajua jinsi Sikukuu ya Lamu ya kusherehekea utamaduni inasherehekewa nchini Kenya.
Je, unafahamu ni kwa nini mji wa Lamu unapatikana katika orodha ya tamaduni za dunia?
Tutawaonyesha jibu la swali hili mwishoni mwa video hii.
Katika sherehe hizi ngoma hupigwa, nyimbo za kitamaduni huchezwa na watu hukatika huku wakivalia mavazi za kimila. Bidhaa za kipekee za kuundwa kwa mikono huonyeshwa ambazo ni mikeka ya sakafu na ya mezani, vitu vya kuweka mapambo na vyombo vingine ndogo ndogo, madoido ya kuweka kwa ukuta za nyumba na hata sahani za kuchagulia chakula na zingine zingi.
Waandalizi wa sherehe hizi hutayarisha mashindano kwa maji na pia kwa nchi kavu, mashindano ya mchezo wa Bao ikipendwa na wengi. Bao, ni mchezo wa waswahili ambao hutumia kipande cha mbao na changarawe na huwavutia watu kutoka ndani na nje ya nchi. Michezo nyingine ni ya mashindano ya punda na mashindano ya jahazi.
Katika sherehe hizi kuna maonyesho ya ukariri wa mashairi ya Kiswahili. Waswahili pia wanapenda kujichora na henna kwa mikoni na miguu ili kujirembesha; haswa wanapojiandaa kufanya harusi. Katika tamasha hizi, sherehe za arusi na miziki ya waswahili huwafurahisha wageni sana.
Mji wa Lamu hutumika kuandaa sherehe ya kiislamu ya Maulidi, ambayo ni sikukuu mjini Lamu ya kusherehekea utamaduni; pia kuna sherehe ya wapaka rangi wa kila mwaka kutoka kote duniani.
Na sasa nitawapa jibu la swali la hapo awali.
Je unafahamu ni kwa nini mji wa Lamu unapatikana katika orodha ya tamaduni za dunia?
Kwa sababu ya kuwepo kwa funguvisiwa kwa Lamu inayopatikana katika orodha maarufu. Lamu lipo katika bahari Hindi kaskazini mwa Kenya. Lamu ipo mahala pengi pa historia za kina. Utamaduni na historia za waswahili huonekana dhahiri kupitia mahala hapa.
Funzo hili lilikuwaje? Je, ulijiifunza jambo lolote la kusisimua?
Je, nchini mwenu kuna sherehe za utamaduni na kama ndio, unapenda kuhudhuria na kujionea mwenyewe?
Tuwachie maoni yako katika SwahiliPod101.com kisha tuonane katika somo lifuatalo!

Comments

Hide