Hamjamboni, mimi ni Medina. |
Sikukuu ya Muziki Nchini Kenya hufanyika jijini Nairobi katika Jumba Kuu la Mikutano la Kimataifa la Kenyatta lililoko katika barabara ya Harambee. Tamasha hii hutendeka mwezi wa nane wa kila mwaka wakati ambapo sekta ya burudani huvuma sana. Wachezaji muziki tofauti hujitokeza na vile vile mashabiki wao. |
Somo hili litakujulisha jinsi Wakenya husherehekea sikukuu hii ya muziki. |
Je, unajua wafadhili wakuu wa tamasha hili ni akina nani? |
Tutawaonyesha jibu la swali hili mwishoni mwa video hii. |
Wizara ya mambo ya kinyumbani na urithi wa nchi huandaa sherehe za muziki wa kinyumbani ambapo hakuna uhusiano wowote na mashule. Vitengo vya serikali na vilabu vya nyumbani, mashirika ya kiserikali ndio wahusika wakuu wa tukio hili. Wao huandaa dansi za kitamaduni, muziki wa kale na pia sarakasi. |
Mabingwa wa muziki kutoka shule za msingi, upili na vyuo vikuu kutoka sehemu mbalimbali nchini hufanya vitengo kadha za muziki na dansi. Vitengo hizi ni kama kipande cha usanii cha kujitungia, nyimbo za kale, nyimbo za pamoja ama kwaya na vipande asili za muziki. Tukio hili la wanafunzi huwa limetayarishwa na wizara ya elimu nchini. |
Washindi katika tamasha hii hufanya maonyesho ya usanii wao mbele ya Rais wa Kenya katika ikulu. Kazi yao hutuzwa taji ya kwaya ya mwaka ya utamaduni nchini Kenya na hualikwa kutumbuiza umati kila wakati kuna sherehe za sikukuu ya kitaifa. |
Wakati wa tamasha hii ya muziki wa kikenya, chakula cha asili kutoka kabila au kundi tofauti nchini Kenya huonyeshwa. Mikahawa tofauti pia hufanya maonyesho ya chakula cha kimataifa kinachotambulika ili kuenda pamoja na muziki. |
Na sasa nitawapa jibu la swali la hapo awali. |
Je, unajua wafadhili wakuu wa tamasha hii ni akina nani? |
Wizara ya elimu pamoja na wizara ya mambo ya nyumbani na urithi wa kitaifa ndio wafadhili wakuu wa tamasha hili. Kama tunavyoona katika maelezo haya, serikali huhusika kwa njia kubwa hata ingawa mashirika ya kibinafsi pia huhusika. |
Funzo hili lilikuwaje? Je, ulijiifunza jambo lolote la kusisimua? |
Je, kuna tamasha kama hili la kila mwaka nchini mwenu? |
Tuwachie maoni yako katika SwahiliPod101.com kisha tuonane katika somo lifuatalo! |
Comments
Hide