Dialogue

Vocabulary (Review)

Learn New Words FAST with this Lesson’s Vocab Review List

Get this lesson’s key vocab, their translations and pronunciations. Sign up for your Free Lifetime Account Now and get 7 Days of Premium Access including this feature.

Or sign up using Facebook
Already a Member?

Lesson Transcript

Hamjamboni, mimi ni Medina.
Katika Sikukuu ya Kimataifa ya Kuhadithiana ya Sigana, wasimulizi kutoka kote duniani huungana pamoja na kushirikiana kwa kuhadithi ngano za kale, na za ushauri na kuelezea shida na ushindi wa watu weusi wanaoishi nchi za kigeni. Ilianzishwa kusherehekea utamaduni wa Kenya.
Funzo hili litatuangazia kinachoendelea katika sikukuu hii ambayo husherekewa na wasimulizi kutoka nchi za Asia, Ulaya, Afrika na kwingineko.
Je, unajua ni wakati upi ambapo tafrija ya kusimuliana hadithi huwa na msisimuko mkuu zaidi?
Tutawaonyesha jibu la swali hili mwishoni mwa video hii.
Kila anayehudhuria lazima awe na tiketi ambazo huuanzwa mbeleni kabla ya siku ya sherehe. Katika maonyesho ya kufungua sherehe hizi, wasimulizi wote wanatambulishwa na kutengewa siku ya kwanza ili wahadithi kwa wasanii wenzao katika maneno, muziki na pia kudansi katika ukumbi.
Siku ya pili ya sherehe hizi huwa inahusika na maonyesho ya jamaa. Tukio hili hufanyika mahala tofauti kama vile ukumbi wa usanii nchini au katika jumba la Utamaduni au Alliance Francaise ambako usanii wa kitaifa hufanyika sanasana. Msimulizi wakimataifa aliye katika kitengo cha familia, na watoto husimulia hadithi zao kwa muziki, maneno na kucheza ngoma.
Waandalizi wa sherehe hizi pia huhushisha wanafunzi wa shule ya upili. Sherehe hizi za wasimulizi sana sana hufanyika katika shule ya upili ya wasichana ya Alliance. Sherehe hizi hufanyika siku nzima wala si kwa masaa machache kama tulivyoongea hapo awali. Wanafunzi tofauti husimulia hadithi zao kwa muda waliopewa. Baadaye maswali huulizwa na waliohudhuria. Kila msimulizi anaweza simulia hadithi yake mara tatu kulingana na vile itapendeza wahudhuriaji.
Wasimulizi wa hadithi na mashabiki wao wanapopatana kwa sherehe hizi kila mmoja wao huwa makini kusoma kutoka kwa mwingine. Kumbuka kuwa watu wa umri wowote huweza kusherehekea na kusoma kupitia muziki, kucheza ama utendaji.
Na sasa nitawapa jibu la swali la hapo awali.
Je unajua ni wakati upi ambapo tafrija ya kusimuliana hadithi huwa na msisimuko mkuu zaidi?
Wasimulizi wengi na mashabiki wao hupenda msisimko unaoletwa na uoga wa hadithi za mapepo. Msisimuko unaongezeka sana kwa sababu ya muda ambao umetengwa kusimulia hadithi hizi, mara nyingi ukiwa katikati ya usiku.
Funzo hili lilikuwaje? Je, ulijiifunza jambo lolote la kusisimua?
Utamaduni wa usimulizi wa hadithi umefika wapi katika nchi yenu?
Tuwachie maoni yako katika SwahiliPod101.com kisha tuonane katika somo lifuatalo!

Comments

Hide