Hamjamboni, mimi ni Medina. |
Sikukuu ya wapendanao ama Valentine husherehekewa kote duniani hata nchini Kenya. Sikukuu hii hufanyika mnamo tarehe 14 mwezi wa pili kila mwaka. |
Fundisho la leo ni la kuelimisha jinsi Wakenya husherehekea sikukuu ya wapendanao. |
Je, unafahamu ni rangi ipi kwa jumla hutumika kusherehekea sikukuu hii? |
Tutawaonyesha jibu la swali hili mwishoni mwa video hii. |
Mkesha wa siku ya wapendanao, watu hujiandaa na kununua zawadi mbalimbali za kuwapa wapenzi wao. Wafanyabiashara hunufaika zaidi kwa sababu ya utamaduni ya watu kutumia pesa kuwafurahisha wapenzi wao. Hii tamaduni imekuwa tangu jadi. Mikahawa, maduka na pia wachuuzi huuza bidhaa na kupeana huduma kwa bei nafuu. |
Siku ya wapendanao inapotimia mtu na mpenziwe hushiriki katika kutuma ujumbe mfupi kwa njia ya simu ama kwa vifaa vingine vya kimitambo (teknolojia) kama vile tarakilishi. Wasichana sanasana hupokea maua ya waridi kutoka kwa waume wao. Maua hutumwa maofisini hata manyumbani kupitia mashirika ya maua. |
Jioni, wanaume huwaalika wapenzi wao wasichana kwa chakula cha jioni. Wasichana huvalia nguo za jioni na kukutana na wanaune ambao huwa wamevaa mavazi ya kupendeza kweli kweli. Wawili hao hula pamoja na kunywa mvinyo na baadaye hubadilishana zawadi. Kila mpenzi hutarajia kuwa mwenzake atampa mapenzi ya hali ya juu. |
Ni ukweli ya kwamba millioni thelathini na tano za bidhaa za chokoleti zenye umbo wa moyo huuzwa siku hii. Chokoleti za zaidi ya dola billioni moja pesa taslimu hununuliwa kwa siku moja pekee yake. |
Na sasa nitawapa jibu la swali la hapo awali. |
Je, unafahamu ni rangi ipi kwa jumla hutumika kusherehekea sikukuu hii? |
Rangi nyekundu ni rangi ya mapenzi na ndiposa watu huonelea ni heri kuitumia kwa sikukuu hii. Mavazi na pia maua na vitambaa kwa mikahawa huwa zote ni nyekundu. Barabara za majiji huwa zimefurika bidhaa nyekundu za wachuuzi. |
Funzo hili lilikuwaje? Je, ulijiifunza jambo lolote la kusisimua? |
Ni mtindo upi ambao hutumiwa sana kusherehekea sikukuu ya wapendanao katika nchi yenyu? |
Tuwachie maoni yako katika SwahiliPod101.com kisha tuonane katika somo lifuatalo! |
Comments
Hide