Dialogue

Vocabulary (Review)

Learn New Words FAST with this Lesson’s Vocab Review List

Get this lesson’s key vocab, their translations and pronunciations. Sign up for your Free Lifetime Account Now and get 7 Days of Premium Access including this feature.

Or sign up using Facebook
Already a Member?

Lesson Transcript

Hamjamboni, mimi ni Medina.
Ijumaa kuu ni sikukuu ambayo wakristo kote duniani hushirikiana katika ukumbusho wa kufa kwake Yesu Kristo. Ni siku ya maana kwa kuwa waumini huamini kuwa Yesu Kristo alisulubiwa msalabani kwa ajili ya dhambi zao ndiposa wakaokolewa.
Fundisho hili litaangazia jinsi Wakristo nchini Kenya hukumbuka kufa kwake Yesu Kristo katika siku hii.
Je, unajua ni matendo gani ambayo wakenya hufanya katika sikukuu hii?
Tutawaonyesha jibu la swali hili mwishoni mwa video hii.
Watu hukumbuka kusulubiwa kwa Yesu Kristo kwa njia tofauti kulingana na imani yao. Katika siku hii takatifu ibada ya ukumbusho huaza saa tisa jioni, masaa ambayo Yesu Kristo alikufa. Katika ibada hii watu hubeba njia ya msalaba na kuupokea mwili wa Kristo.
Wakristo wengi hufunga na kujinyima chakula; Wakila, wao hula mkate pekee yake ili kukumbuka mateso aliyopitia mwana wa mungu. Waumini wa kanisa la kikatoliki huomba kwa Rosari. Wao hutubu na kumshukuru mungu kwa kumtoa mwana wake wa pekee.
Hata kama wakristo wengi huitazama Ijumaa hii kama ijumaa ya msiba mkuu, watu huwaalika wawapendao ambao ni jamaa na marafiki kwa manyumba zao. Wao huwaandalia chai na mikate moto yenye umbo wa msalaba. Kwa watu ambao hawajihushisi sana na mambo ya dini, Ijumaa kuu ni likizo ya kawaida ambayo wao hula na kunywa kwa njia za kidunia.
Wakristo wengi hukula samaki na mboga za rangi ya kijani kibichi katika sikukuu hii ambayo huchukuliwa kama siku ya mazishi. Ni siku ya huruma na ya kudhamiria kwa kwingi.
Na sasa nitawapa jibu la swali la hapo awali.
Je, unajua ni matendo magani ya kiroho ambayo watu hufanya katika sikukuu hii?
Wakristo wengi hutumia siku hii kutafakari na kuwaza jinsi Kristo aliuawa kwa msalaba. Wao huomba, kufunga na kutubu dhambi ili kufanikisha uhusiano wao na mungu.
Funzo hili lilikuwaje? Je, ulijiifunza jambo lolote la kusisimua?
Je, watu wa nchi yako husherehekea Ijumaa kuu vipi?
Tuwachie maoni yako katika SwahiliPod101.com kisha tuonane katika somo lifuatalo!

Comments

Hide