Hamjamboni, mimi ni Medina. |
Sikukuu hii ya kupeana vijisanduku husherehekewa nchini Kenya na kote duniani mnamo tarehe 26, ambayo ni siku moja baada ya sikukuu ya Krisimasi. |
Fundisho hili linatoa elimu ya jinsi Wakenya husherehekea siku ya kupeana vijisanduku. |
Je, sikukuu hii ni siku ya kurudisha zawadi ambazo hazitii fora kama wanavyodhania baadhi ya wakenya? |
Tutawaonyesha jibu la swali hili mwishoni mwa video hii. |
Sherehe ya kupeana vijisanduku huanza na kufunga zawadi katika vijisanduku ili kuwapea watu waliokusaidia kwa njia moja au nyingine katika mwaka huo. Watu hawa wanaweza kuwa msusi wako wa nywele, mtu akulimiaye kwa bustani ama mtu mwingine yeyote ambaye alikufaa kwa dhiki. Zawadi pia hupewa watu ambao hawajafanikiwa sana maishani. |
Watu wa jamaa moja, kanisa moja au waliokuwa na ushirikiano fulani hushiriki katika tafrija za michezo kama vile kadanda au kriketi. Ikiwa hali ya anga inaruhusu, wao huenda kupanda milima mojawapo ikiwa mlima Kenya au kuamua kutembea pamoja wakitazama mazingira na kupiga domo. Wao hula chakula maalum wakipendacho, mara nyingi ikiwa chakula walichobakisha katika sikukuu ya Krisimasi. Siku hii watu hualika marafiki na jamaa wengi kwa nyumba zao na wengine huchagua siku hii kufungua nyumba zao mpya. |
Jamaa na marafiki huenda kununua bidhaa baada ya kula na kuhusika kwenye michezo. Wao huchukua nafasi hii kupata vitu vilivyokuwa vya bei nafuu wakati wa Krisimasi. Bidhaa hizi mpya hutumika kama zawadi kwa sababu mada ya siku hii kuanzia macheo hadi machweo ni kupeana na usamaria mwema. Baadaye watu huenda kujionea mashindano ya michezo. |
Sikukuu hii haina uhusiano wowote na mchezo wa kupigana mangumi vile watu wengi wanafikiria kulingana na jina 'boxing.' Mafukara hupata kupokea zawadi na pia matajiri hupata fursa ya kuwafikiria wanyonge. |
Na sasa nitawapa jibu la swali la hapo awali. |
Je, hii ni siku ya kurudisha zawadi ambazo hazitii fora kama walivyodhania baadhi ya wakenya? |
La hasha, hii sio siku ya kurudisha zawadi ambazo hazipendezi kwa waliozituma siku ya Krisimasi. Ni siku ambayo zawadi kama kadi, vikombe, shati, mikoba, mapambo na nyinginezo hupeanwa. |
Funzo hili lilikuwaje? Je, ulijiifunza jambo lolote la kusisimua? |
Je, siku ya vijisanduku ni sikukuu ya serikali nchini mwenu? |
Tuwachie maoni yako katika SwahiliPod101.com kisha tuonane katika somo lifuatalo! |
Comments
Hide