MTO NA CHANZO |
Hiki ni kitabu cha kuwezesha na wengi wanakiona kama wito wa uamsho hasa kwa wanawake. |
Hadithi hii inagusia vizazi vitatu vya kitamaduni na ya kisasa ya wanawake wa jamii ya wajaluo. |
Wahusika wakuu ni Akoko aliyezaliwa katika jamii ya utamaduni ya waluo, na mjukuu wake Awiti ambaye ameangazika pamoja na watoto wake wanaoishi katika karne ya ishirini na mmoja. |
Hadithi hii ya kuvutia huanza na hadithi ya mapenzi ambapo Akoko, binti wa pekee wa chifu mkuu amefikia umri wa kuolewa. |
Kuna waposa wengi wanaotakakumchumbia. |
Mmoja wao amempenda zaidi hadi amekubali kulipa mahari ya ngo'mbe thelathini, kiwango cha juu sana wakati huo ambapo watu wachache wangemudu. |
Aliolewa na ndoa yao ilikuwa yenye raha hasa baada ya kupata watoto kama baraka ya Were aliyekua mungu wa jua. |
Hata hivyo, furaha hii haikuendelea kwa muda mrefu. |
Mumewe alifariki na kumwacha pamoja na wanawe. |
Matatizo yake yalianza wakati familia ya mumewe iliamua kumnyanganya mali aliyoachiwa. |
Akoko alichukua hatua na kwenda kwa serikali ambayo kwa wakati huo ilikuwa ya wa wazungu. |
Aliomba msaada, jambo ambalo halikuwa limefanywa na mtu yeyote. |
Juhudi zake hazikuwa za bure kwani alisaidiwa baada ya uchunguzi na mali yake kurejeshwa. |
Bintiye, ambaye kwa sasa pia ni mjane alianza kuteswa na familia ya mumewe na akaamua kuenda kutafuta msaada kutoka kwa mungu anayewasaidia wajane na mayatima. |
Alienda hadi kwa kanisa ya misheni ya katoliki na kujiunga na imani yao. |
Mamake na dadake Awiti pia walijiunga naye. |
Awiti ni mwerevu na yuko miongoni mwa wasichana wawili wanaodhaminiwa kupata masomo katika koleji ya uwalimu. |
Baadaye anaoleka na kupata watoto saba ambao wanapata mafunzo ya utaalamu kama vile uhudumu wa hewa na utoaji damu. |
Comments
HideMTO NA CHANZO
Hiki ni kitabu cha kuwezesha na wengi wanakiona kama wito wa uamsho hasa kwa wanawake.
Hadithi hii inagusia vizazi vitatu vya kitamaduni na ya kisasa ya wanawake wa jamii ya wajaluo.
Wahusika wakuu ni Akoko aliyezaliwa katika jamii ya utamaduni ya waluo, na mjukuu wake Awiti ambaye ameangazika pamoja na watoto wake wanaoishi katika karne ya ishirini na mmoja.
Hadithi hii ya kuvutia huanza na hadithi ya mapenzi ambapo Akoko, binti wa pekee wa chifu mkuu amefikia umri wa kuolewa.
Kuna waposa wengi wanaotakakumchumbia.
Mmoja wao amempenda zaidi hadi amekubali kulipa mahari ya ngo'mbe thelathini, kiwango cha juu sana wakati huo ambapo watu wachache wangemudu.
Aliolewa na ndoa yao ilikuwa yenye raha hasa baada ya kupata watoto kama baraka ya Were aliyekua mungu wa jua.
Hata hivyo, furaha hii haikuendelea kwa muda mrefu.
Mumewe alifariki na kumwacha pamoja na wanawe.
Matatizo yake yalianza wakati familia ya mumewe iliamua kumnyanganya mali aliyoachiwa.
Akoko alichukua hatua na kwenda kwa serikali ambayo kwa wakati huo ilikuwa ya wa wazungu.
Aliomba msaada, jambo ambalo halikuwa limefanywa na mtu yeyote.
Juhudi zake hazikuwa za bure kwani alisaidiwa baada ya uchunguzi na mali yake kurejeshwa.
Bintiye, ambaye kwa sasa pia ni mjane alianza kuteswa na familia ya mumewe na akaamua kuenda kutafuta msaada kutoka kwa mungu anayewasaidia wajane na mayatima.
Alienda hadi kwa kanisa ya misheni ya katoliki na kujiunga na imani yao.
Mamake na dadake Awiti pia walijiunga naye.
Awiti ni mwerevu na yuko miongoni mwa wasichana wawili wanaodhaminiwa kupata masomo katika koleji ya uwalimu.
Baadaye anaoleka na kupata watoto saba ambao wanapata mafunzo ya utaalamu kama vile uhudumu wa hewa na utoaji damu.